Pages

Wednesday, May 15, 2013

ROONEY AJADILIWA KWA DAKIKA 90 HOTELINI NA MAN UTD KUMRUDISHA CESC FABREGAS




LONDON, England
KOCHA Mkuu Mpya wa Manchester United, David Moyes, ameweka bayana mipango yake kwenye klabu hiyo kwamba anamtaka Wayne Rooney aendelee kuwepo.
Na kutokana na matakwa ya mshambuliaji huyo, Rooney kutaka kuondoka, jambo hilo liliwafanya Moyes, Alex Ferguson na Ryan Giggs kukutana Alderley Edge — kwa ajili ya mazungumzo juu ya kuweza kumaliza tatizo la fowadi huyo ili aendelee kubaki Old Trafford.
Moyes, Fergie na Giggs walipigwa picha wakiwa wanatoka pamoja katika Hoteli ya Alderley Edge, ambapo walikutana saa 4.30 asubuhi na kuwa na mazungumzo yaliyodumu kwa dakika 90. Shuhuda aliyeona tukio hilo, watatu hao walipokuwa wanatoka kwenye hoteli hiyo walikuwa wakipepesa macho pande zote kuona kama hakuna aliyewaona.
@@@@@@@

Man Utd kumrudisha England kiungo Fabregas

BARCELONA, Hispania
MABINGWA wa soka wa England, Manchester United, wamepanga kuushitua ulimwengu kwa kumsajili kiungo wa Barcelona, Cesc Fabregas.
London Evening Standard lilibainisha kwamba United imepanga kumtengenezea mazingira mazuri kocha mpya wa timu hiyo, baada ya Sir Alex Ferguson kutangaza kustaafu na sasa wanamshusha Fabregas Old Trafford, ikiwa si muda mrefu tangu alipohama kutoka Arsenal kwenda Barca.
Inaaminika kwamba tayari mawasiliano yameshafanywa baina ya United na Barca juu ya Fabregas, ambaye aliondoka Emirates Stadium kwa ada ya pauni milioni 35 miaka miwili iliyopita.
Barcelona bado hawajailipa Arsenal pauni milioni tano na hivyo watakuwa tayari kumwachia kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania kwa dau la pauni milioni 20.
Fabregas ameshindwa kuonyesha makali yake katika klabu hiyo ya Nou Camp na jambo hilo limemfanya kuwa kwenye lawama nyingi kutoka kwa mashabiki wa timu hiyo, kutokana na kiwango chake cha msimu huu.
Iliripotiwa kwamba Arsenal imeweka kipengele kwenye mkataba wake wakati inamuuza Fabregas kwenda Barca kwamba inaruhusa ya kumnunua kama itahitaji hivyo na Januari mwaka huu, kocha Arsene Wenger aliamini kwamba nahodha wake huyo wa zamani atarudi Emirates siku moja.
“Sishawishiki kuamini kwamba siku moja hatarudi hapa kwa sababu yeye ni mtu wa Arsenal. Anaipenda Arsenal, amekuwa akitazama kila mechi ya Arsenal,” alisema bosi huyo wa Washika Bunduki.

No comments:

Post a Comment