Pages

Friday, May 24, 2013

RONALDO, MOURINHO WAFUNGIWA MECHI MBILI,KUKU MOURIHNO AKIELEKEA DARAJANI!!!

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo na kocha wake Jose Mourinho wamefungiwa mechi mbili za michuano ya Kombe la Mfalme baada ya kutolewa nje katika fainali dhidi ya Atletico Madrid. Mourinho mwenye umri wa miaka 50 alitolewa nje baada ya kumshambulia mwamuzi kwa maamuzi aliyotoa adhabu ambayo hataweza kuitumikia baada ya kutangaza kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu.Ronaldo mwenye umri wa miaka 28 alipewa kadi nyekundu baada kukutwa na hatia ya kumpiga teke la uso kwa makusudi mchezaji wa Atletico, Gabi. Wote wawili Ronaldo na Mourinho watakuwepo katika michezo miwili ya mwisho ya ligi ya Madrid.

No comments:

Post a Comment