Pages

Sunday, May 19, 2013

NZERA KITANO ATWAA TAJI LA REDD'S MISS KIBAHA 2013


Redds Miss Kibaha 2013, Nzera Kitano (katikati) akiwa na washindi wenzake mshindi wa pili, Ester Albert (kushoto) na Rachel Joh, baada ya kutangazwa washindi katika shindano lao lililofanyika juzi Ijumaa usiku kwenye Ukumbi wa Kibaha Kontena. 



ALIYEKUWA mshiriki namba 6 katika shindano la kumsaka Redds Miss Kibaha 2013 Nzera Kitano ameibuka kua Redds Miss
Kibaha 2013 katika shindano lililofanyika kwenye ukumbi wa Conteainer Kibaha Maili Moja mkoani Pwani.
Nzera ambae alionekana kuwa mchezi tangu mwanzo wa shindano aliweza kupenya katika hatua ya nusu fainali ambapo aliingia katika warembo watano bora kati ya washiriki 10 waliokuwa wakishindana kuwania taji hilo.

Aidha kwa ushindi huo Nzera amepata zawadi ya fedha taslimu sh.300,000 pia amepa ofa ya kwenda kuchagua vipodozi na mapambo ya aina mbalimbali katika duka la Shear Illusion lilipo Mlimani City pamoja na king’amuzi kutoka kampuni ya Multichoice ambapo atafungiwa bure.
Mshindi wa pili ni Ester Albert ambaye amepata fedha taslimu kiasi cha sh.200,000 pia atapata ofa ya kulipiwa ada ya shule au kutafutiwa kazi na mdau ambaye hataki kutaja kwenye vyombo vya habari.

Mshindi wa tatu ni Rachel John aliyepata fedha taslimu sh. 150,000 huku nafasi ya nne ikienda kwa Sylvia John huku nafasi ya tano ilikwenda kwa Beatrice Bahaya.
Kwa ushindi huo warembo wote watano wamepata nafasi ya kwenda kushiriki kwenye shindano la Redds Miss Pwani watakakochuana na warembo wa Bagamoyo kuwania tiketi ya kwenda kushiriki katika shindano la Kanda ikiwa ni katika kuwania tiketi ya shindano la taifa.

No comments:

Post a Comment