Pages

Tuesday, May 28, 2013

NIKO TAYARI KUFANYA CHOCHOTE CRISTIANO RONALDO ABAKI BERBABEU

clip_image001[6]Dili kweli: Perez anajiandaa kubomoa benki ili Ronaldo abaki Realclip_image001
Rais wa Real, Perez anataka Ronaldo abaki na Bale atue Bernabeu


RAIS wa Real Madrid, Florentino Perez anajiandaa kumfanya Cristiano Ronaldo awe mchezaji anayelipwa zaidi duniani katika jithada za kumshawishi abaki Bernabeu, baada ya kuondoka kwa Jose Mourinho.
Perez amesema: "Ningependa Cristiano Ronaldo awe mchezaji anayelipwa zaidi duniani. Tunakwenda kufanya kila kitu katika mikono yetu kumfanya awe na furaha.’
Nyota huyo wa zamani wa Manchester United amekuwa akihusishwa na uvumi wa kurejea Old Trafford msimu ujao au kwenda kujiunga na Matajiri wa Ufaransa, Paris Saint-Germain - lakini Perez anapambana kumzuia Madrid kwa muda zaidi.
Ronaldo amekuwa mchezaji mkubwa duniani tangu anunuliwe kwa Pauni Milioni 80 kutua Hispania mwaka 2009, akifunga mabao 146 katika mechi 135.
Rais wa Madrid pia amesema kwamba licha ya matatizo yote yaliyotokea na Special One msimu huu, wachezaji bao wanamzungumzia vizuri Mourinho.
Alisema: "Wachezaji wanamzungumzia vizuri tu Mourinho. Wameniambia alikuwa bora. Hatujui nani atakuwa kocha mpya. Tutazungumzia hilo wiki ijayo. Lakini tunataka Zinedine Zidane awe kiongozi wa mpango huu,"alisema.
Kazi ya kwanza ya Zidane ni kuhakikisha anamsajili nyota wa Tottenham, Gareth Bale kwa Pauni Milioni 65.

No comments:

Post a Comment