Pages

Wednesday, May 29, 2013

MSANII IRYN NAMUBIRU WA UGANDA AWASHUKURU MASHABIKI KIPINDI ALICHOKUWA ANASHIKILIWA KWA TUHUMA ZA MADAWA YA KULEVYA


Baada ya kunusurika katika mikono mikali ya sheria nchini Japan, Msanii wa muziki Iryn Namubiru hatimaye kwa njia ya mtandao amesema na mashabiki na watu wote ambao wamekuwa nyuma yake wakati wa tatizo lililompata ambapo ametoa shukrani kwa sapoti na pia kukanusha kuongea na chombo chochote cha habari juu ya ishu hii nzima.
Kufuatia taarifa mbalimbali kuendelea kusemwa kuhusiana na tukio hili, Iryn amesema kuwa atatoa maelezo kamili wakati ukifika, na kidogo alichosema kuhusiana na hili ni kuwa, katika tukio hili hakufunguliwa mashtaka rasmi na hakufikishwa mbele ya Jaji.

No comments:

Post a Comment