Pages

Friday, May 31, 2013

MOURINHO ASAINI MIAKA MINNE CHELSEA

London, England

JOSE MOURINHO sasa ni kocha mpya wa Chelsea, baada ya Jumanne wiki hii kukubali kusaini miaka minne ya kuinoa klabu hiyo.

Mkataba huo wa miaka minne wa 'The Special One' utamfanya ajikusanyie pauni milioni 40 kama mshahara wake.

Chanzo kikuu cha Blues, kiliweka wazi: “Ni rasmi sasa Jose ni kocha tena wa Chelsea! Kila mmoja amekubaliana na ujio wake mara nyingine tena, klabu, wachezaji na hata mashabiki.

“Kwa sasa tunatazama mbeleni kwa msimu ujao, tunauhakika utavutia sana.”


Mei 3, mwaka huu Gazeti la 'The Sun' ndilo lililokuwa la kwanza kueleza kwamba kocha huyo wa Real Madrid, Mourinho atatua Stamford Bridge na sasa limeeleza tena kwamba, tayari Mreno huyo amesaini mkataba rasmi wakati alipofanya safari mara mbili jijini London wiki hii.

No comments:

Post a Comment