Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, May 15, 2013

KWA HILI HUTAONA HURUMA KWANINI MANCINI AMEONDOSHWA MAN CITY


Waving goodbye to Manchester: But where will Roberto Mancini end up next?
MANCHESTER, England
MWISHOWE, kama inavyoonekanakwa sasa, Roberto Mancini amesalitiwa na maneno yake mwenyewe. Baada ya kikosi chake ghali kabisa kiliposambaratishwa na Wigan Athletic yenye wachezaji wa kawaida kabisa, bosi huyo wa Man City anayelipwa pauni milioni saba kwa mwaka, aliulizwa kitu gani kimekwenda kombo kwenye mchezo huo.

“Hatukucheza vizuri sana,” hilo likawa kisingizio chake. Na kwanini hawakucheza vizuri? Akajibu: “Sijui.”
Hii ni hatari. Kama kocha hafahamu kwanini wamefungwa, nani  atafahamu sasa? Haya ndio maneno ambayo yatameponza Mancini.

Baadaye akaibuka na kudai kwamba mabosi wake aliokuwa akifanya nao kazi kwa karibu, hawajampa ulinzi wa kutosha — lakini ukweli wa mambo Muitaliano huyo aliathiriwa na uvumi wa hatima ya kibarua chake.
Sasa tunaweza kuona kwanini kocha huyo hakuhakikishiwa ulinzi. Tayari alitambua kwamba siku zake zinahesabika katika klabu hiyo, lakini alishindwa kuonyesha ushawishi ambao ungeweza kubadili hali ya mambo katika dakika za mwisho.

Na tayari kwasababu yeye mwenyewe mapema tu alishaanza kuwatupia lawama mabosi wake baada ya mambo kwenda kombo kwenye Ligi Kuu England, vibopa hao hawakuweza kumkingia kifua na ndio wanaomfungulia mlango wa kutoka mahali hapo.

Kitu kingine alikuwa akiwanyenyekea sana wachezaji wake, anawaonyesha nidhamu ya woga — kitu ambacho ni hatari sana kwasababu kilionekana wazi kwamba hana uwezo wa kimbinu zaidi ya kuwategemea wachezaji wake hao wafanye mambo ndani ya uwanja.
Kile kilichotokea Jumamosi katika mchezo wa fainali ya Kombe la FA iliyofanyika pale Wembley na kunyukwa 1-0 na Wigan, kilitibua kila kitu. Kwa jinsi alivyo Mancini, atatupia lawama watu wote, lakini wakulaumiwa hapa ni yeye mwenyewe.

Sasa tayari anafungasha kilicho chake na kuelekea mlango wa kutokea na ni watu wachache sana watakaomwonea huruma kwa hilo. Kwa kifupi tu, jina lake lilishaandikwa ukutani kwamba ataondoka tangu timu hiyo ilipoboronga kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.
Sawa, kufika fainali ya Kombe la FA na kumaliza mshindi wa pili kwenye ligi, yangeonekana kuwa ni mafanikio makubwa kwa klabu inapofika mwisho wa msimu.

Lakini, kwa klabu kama Man City, hayo hayakuwa mafanikio ambayo wameyalenga. Man City hii, klabu ambayo imetumia zaidi ya pauni bilioni moja, ambazo bosi wake Sheikh Mansour ameamua kuwekeza hapo.
Hadi hapo, kwa kutazama fedha hizo tu ilizotumia katika shughuli mbalimbali ikiwamo usajili wa wachezaji unaweza kuona hii si timu ambayo inaweza kumaliza msimu bila ya taji lolote.

Wakati Manchester United ilipotwaa taji lake la kwanza baada ya kusubiri kwa miaka 26, msimu uliofuata walinyakua mataji mawili. Lakini, Mancini, ameshindwa kuituliza klabu yake na kuendeleza makali yake baada tu ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu uliopita
Chelsea ilichelewa tu kuzinduka kwenye mchezo wa nusu fainali waliocheza na Man City, ambapo kipindi cha pili ndipo walipoanza kucheza kwa kiwango kikubwa, lakini kama wangeanza tangu filimbi ya kwanza, sidhani kama Man City ingeweza kufika fainali ya Kombe la FA.

Mapema tu, msimu huu walitupwa nje ya michuano ya Kombe la Ligi na Aston Villa, tena kwa kichapo cha mabao 4-2 nyumbani. Waliondoshwa hatua ya makundi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.
Sawa, unaweza kusema hawakuwa na bahati kwa kupangwa kundi moja na timu za Real Madrid na Borussia Dortmund, lakini bado walikuwa hawana sababu ya kuambulia pointi tatu tu kwenye kundi lake, zikiwa pointi ndogo zaidi ilizowahi kupata timu ya England katika michuano hiyo.
Kufeli kote, Mancini amekuwa akipeleka lawama kwa wachezaji wake, akidai kwamba hana wachezaji wenye viwango vya kufanya yale yanayotakiwa.

Lakini, wakati tukilitazama hilo, nani alimsajili Samir Nasri, Edin Dzeko na aliyekuwa akimchekea Mario Balotelli?
Nani aliamua kumwaanzisha Balotelli kwenye mechi ya Manchester derby badala ya Carlos Tevez? Balotelli huyo huyo, wastani wake anafunga bao moja kila baada ya dakika 535, unatumia akili gani hapa kumweka nje Tevez, mtu ambaye amekuwa na wastani mzuri wa kufunga tangu alipoondoka Old Trafford?

Lakini, Mancini alishindwa kuliona hilo, hadi timu yake ilipokuwan nyuma kwa mabao 2-0 ndipo alipomwingiza Tevez na Muargentina huyo aliweza kubadilisha hali ya mchezo. Sawa, kwa kuwa Man City bado ilipoteza mechi hiyo kwa bao la dakika za mwisho la Robin van Persie, lakini Tevez alionyesha wazi kwamba kocha wake alifanya kosa la kiufundi.

Baadaye akaangushwa na safu yake ya ulinzi — jambo hili liliwagharimu zaidi katika Ligi ya Mabingwa barani Ulaya. Baada ya kuona safu hiyo inaruhusu sana mabao, hakutafuta suluhu na badala yake alianza kumshushia lawama kipa Joe Hart, huku akiwa amesahau kwamba miezi sita iliyopita alimsifu kwamba ni kipa bora aliyepata kutokea nchini England.

Baadaye likaja tatizo la kutibuana na Vincent Kompany na James Milner, wakati huo huo ikumbukwe kwamba Nigel de Jong aliondoka Man City kwasababu ya Mancini. Bado kuna tatizo linalomhusu Joleon Lescott.
Wachezaji ambao walishindwa kumwelewa kocha huyo, walishachoka na kwamba walikuwa tayari kwa lolote litakalomtokea. Mancini, hakuwa amejitazama mwenyewe.
Klabu ikaingia kwenye hasara nyingine kwa kufanya usajili ulioighatimu klabu pauni milioni 40 kuwasajili Javier Garcia, Jack Rodwell, Scott Sinclair na Maicon, ambao walikuwa 'mizigo' tu katika klabu hiyo.
Haya nani aliwasajili hawa? Kitu kingine, kumlealea Balotelli hakujua kuwa hiyo ni sumu aliyokuwa anaiweka kwenye vyumba vya kubadilishia nguo? Mancini ametibua mambo mwenyewe.

Ilipofika Jumamosi jioni, Mancini alijibu uvumi  wa kuondoka kwake kwamba ni “pumba” kwa maana waliokuwa wakieneza uvumi huo ni “wajinga” — lakini baadaye akaelewa, akasema: “Au, kama ni kweli, nitakuwa mjinga kwa kutoelewa.” Hapa alielewa kilichokuwa kikizungumza.
Kabla ya fainali hiyo akasema: “Kama tutashinda taji hilo, watu wengi watasema tumekuwa na msimu mzuri. Lakini, pale Inter nilitwaa mataji saba katika kipindi cha miaka minne na bado walinitimua.”

Na sasa kibarua chake Etihad kimeota mbawa, akisubiri kurithiwa na Manuel Pellegrini, kocha wa Malaga. Imeelezwa kwamba wanasheria wa Pellegrini walishachukua mkataba wa Man City siku kadha zilizopita.
Mancini atakuwa analifahamu hilo, kwasababu hata yeye wakati anasaini kutua Man City, kocha aliyekuwa yupo kwenye timu, Mark Hughes hakuwa anafahamu lolote. Na sasa Mancini atakumbukwa kwenye klabu hiyo kama mtu aliyewapa ubingwa wa Ligi Kuu baada ya kusubiri kwa miaka 44.

Siku moja atakuwa kukiri kwamba aliyetengeneza mazingira ya kufeli kwake ni yeye mwenyewe. Sawa, wachezaji wake walimwangusha Wembley. Kama alivyofanya Jumamosi iliyopita, anapaswa kujiuliza mwenyewe, kulikoni? Pengine hawakuwa wakimpenda na tayari walishasikia tetesi za kuondolewa kwake, hivyo walikubali kufungwa ili kuhitimisha safari yake.

No comments:

Post a Comment