Pages

Friday, May 31, 2013

KONA YA BIG BROTHER AFRICA THE CHASE SEASON 8, MAMBO YAANZA


Neyll, Motamma wategana
MSHIRIKI kutoka Angola, Neyll,  ambaye tangu aingie kwenye Jumba la Diamond amekuwa mkimya imegundulika kumbe ni noma kwa wasichana.
Muangola huyo alikutana na Motamma, lounge mchana wa juzi na kuanza kumpigia misele, Neyll alianza kumuingia Motamma kwa kumuambia: “Unanikumbusha mama yangu.”
Baada ya maneno hayo wawili hao walionekana kuwa karibu sana na kupiga stori za hapa na pale, kabla ya kuanza kucheza muziki kwenye eneo hilo la kupumzikia, wawili hawa kama wakiendelea hivi basi siku si nyingi wataingia mapenzini.
@@@@

Kweli Hakeem noma
HAKEEM amethibitisha kuwa anavipaji vingi, baada ya kuiga sauti ya Biggie alipokuwa kwenye chumba cha mahojiano.
“Hakeem hapa, Big Brother nimefika,” alisema Hakeem akiiga sauti ya Biggie, jambo ambalo lilimvutia Big Brother na kumfagilia mshiriki huyo kutoka Zimbabwe.
Hakeem ambaye yuko kwenye Jumba la Rubies, alitoa tabasamu pana la kujikubali baada ya kufagiliwa na Biggie.
@@@

Presha yamtesa Natasha
MSHIRIKI kutoka Malawi, Natasha, amesema kwamba presha yake imekuwa juu tangu Jumapili walipoingia kwenye mjengo wa Big Brother Africa.
Akiwa kwenye chumba cha kumbukumbu Natasha alimwambia Biggie: “Presha yangu imekuwa juu tangu Jumapili.”
Baada ya kusikia hivyo, Biggie alimwambia kwamba afya za washiriki ni kitu muhimu sana kwa Big Brother.
Tayari daktari ameshamtembelea Natasha kwenye Jumba la Rubies na kumwambia kwamba awe mwangalifu kwa sababu presha yake ilikuwa juu sana.
Kikaangoni
Wiki hii, Denzel, Betty, Hudda, Selly na Natasha mpigie kura mshiriki umpendae abaki mjengoni.


No comments:

Post a Comment