Pages

Monday, May 27, 2013

FALCAO KWENDA MONACO KUPIMWA AFYA LEO.

STRAIKA HATARI wa Atletico Madrid, Radamel Falcao, atapimwa afya yake kwenye Klabu ya Monaco ambayo imepanda Daraja Msimu huu kurudi Ligue 1 ya France na Uhamisho wake unatarajiwa kugharimu Dau la Pauni Milioni 51. 


Habari hizi zimevuja huko Spain na kudaiwa kuwa Atraika huyo kutoka Colombo atapimwa afya yake leo Jumatatu Mei 27.
Monaco, ambayo imenunuliwa na Tajiri wa Kirusi Dmitry Rybolovlev, tayari imeshawanunua Mastaa wa FC Porto Joao Moutinho na James Rodriguez kwa Dau la Jumla ya Pauni Milioni 60 na kutua kwa Falcao kutawafanya watatu hao wakutane tena kwani waliwahi kuchezea Klabu moja.

Kuhama kwa Falcao kulidokezwa na Meneja wa Atletico Madrid Diego Simeone ambae ameshasema hatakuwa na kinyongo ikiwa Falcao, mwenye Miaka 27, atahama.
Hivi Juzi, Kocha Msaidizi wa Monaco, Jean Petit, alidokeza wanatarajia Falcao na Wachezaji wengine wanne au watano wa kiwango chake kununuliwa na Klabu yao.

Mwezi Desemba 2011, Dmitry Rybolovlev alinunua Hisa za Asilimia 60 za Klabu ya Monaco na kuanza kuibadili wakati huo ikiogelea Daraja la chini huko France, Ligue 2, na Mwezi Mei 2012 alimteua Kocha wa zamani wa Chelsea Claudio Ranieri kuiongoza Monaco na amefanya hilo kwa mafanikio kwa kuirudisha Monaco Daraja la juu huko France.

No comments:

Post a Comment