Pages

Wednesday, May 1, 2013

CHEKA AMTANDIKA MASHALI KAMA MTOTO, APOTEZA NETWORK KWA DAKIKA KADHAA

Francis Cheka akiwa ameshavalishwa mkanda wa IBF baada ya kumpiga Thomas Mashali kwa KO raundi ya kumi leo kwenye ukumbi wa PTA Sabasaba, jijini Dar es Salaam

Thomas Mashali akiwa ameanguka nje ya ulingo baada ya kupokea konde zito toka kwa Cheka

Mashali akificha uso kukwepa ngumi nzito za Cheka



Mashabiki wa ngumi wakifuatiliampambano kwa makini

Mashali alizidiwa kila raundi


Mashali akitibiwa baada ya kupigwa ngumi zilizomchana na Cheka

Francis Cheka akiongea na waandishi baada ya mpambano

Thomas Mashali akiongea na waandishi huku akiwa amekaa kwenye kiti

Mashabiki wa Thomas Mashali wakiwa wameduwaaa baada ya kupigwa kwa KO

Hii ilikuwa raundi ya pili tu Mashali akiwa analamba sakafu

BONDIA Francis Cheka amemdunda Thomas  Mashali katika raundi ya 10 katika pambano lao la raundi 12 Ubingwa wa IBF,  lililomalizika muda mchache uliopita kwenye Ukumbi wa PTA, Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mashari ambaye alikuwa na papara za kurusha ngumi ambazo zilipanguliwa vilivyo na Cheka alijikuta akipigwa ngumi na kuanguka kwenye raundi ya pili na kadri muda ulivyokuwa unasonga mbele alishindwa kuhimili vishindo vya bondia huyo wa Morogoro.

Cheka alikuwa na uwezo wa kumpiga kwa KO kwenye raundi ya nne lakini alimpeleka kidogo kidogo ili mashabiki wapate burudani na ilipofika raundi ya 10, Cheka alimtwanga konde lililompeleka Mashali ambaye aliona bora shari kamili na kuamua kukubali kwamba amekwisha.

Kijana huyo wa Manzese alionekana kuwa kama fahamu zilipotea kwani mwamuzi alipokuwa anamsemesha wakati akiwa chini hakuonyesha dalili za kumwelewa na ndipo alipomtoa kilinda meno (teeth guard) ili awe salama.

Kutokana na ushindi huo, Cheka amebeba gari aina ya Toyota Noah ambayo mshindi wa pambano hilo aliahidiwa pamoja na mkanda wa IBF ambao atatakiwa kutetea na bondia Chiokta Chimwemwe wa Malawi.

Awali Mashali alikuwa akitamba kwamba yeye ndiye bondia pekee anayeweza kumchapa Cheka baada ya kuwashinda karibu mabondia wote wanaojulikana nchini kwa kuwa na uwezo mkubwa.

Lakini imeshindikana na sasa imethibitika kwamba Cheka, hana mpinzani nchini hasa baada ya kuwapiga lundo la mabondia wakiwemo wakali kama akina Rashid na Hassan Matumla, Maneno Oswald ‘Mtambo wa Gongo’, Karama Nyilawila na wengine kibao.

No comments:

Post a Comment