Pages

Friday, May 17, 2013

CARRICK AMFUNIKA RVP, AWA MCHEZAJI BORA MAN UNITED



Michael Carrick ametangazwa mchezaji bora wa Manchester United wa mwaka huku mabingwa hao wa ligi kuu England wakiendelea kusherehekea ubingwa wa msimu huu 2012-2013 waliotwaa jumapili iliyopita.

Van Persie

Robin van Persie akiwa na Sir Matt Busby kwenye tuzo za mchezaji bora za United

Carrick alifanya kazi nzuri ya hapo klabuni Manchester United wakati wa msimu huu ambao kocha wao Sir Alex Ferguson amestaafu kuifundisha timu hiyo yenye wapenzi wengi Duniani. Carrick ametwaa tuzo hiyo juzi jumatano dhidi ya mfungaji mabao anayeongoza ligi hiyo inayoishilia ukingoni hivi karibuni Robini Van Persie ambaye pia alibwagwa chini kwenye kinyang'anyiro cha mchezaji bora baada ya Gareth Bale wa Spurs kuchukua tuzo hiyo. Hata hivyo mpaka sasa hakuna anayemfikia RVP kwa ufungaji wa mabao mpaka sasa anaongoza kwa idadi kubwa ya mabao 25. Hata hivyo RVP alipigiwa kura nyingi na Mashabiki pamoja na kufunikwa na Carrick
Ferguson akisalimiana na Robin Van Persie huku wote wakionekana nyuso za furaha

Ferguson akiteta na Jim Rosenthal

Sir Alex Ferguson akiteta jambo na Patrice Evra, Anderson na Antonio Valencia

No comments:

Post a Comment