Pages

Friday, May 24, 2013

Breaking News!!!!! NIYONZIMA ASAINI YANGA MKATABA WA MIAKA MIWILI



Yanga imefanikiwa kushinda vita kubwa ya kufanikiwa kumbakisha kiungo wake, Haruna Niyonzima.

Niyonzima amesaini mkataba wa miaka miwili na kuendelea kubaki Yanga.
Akizungumza na Salehjembe, Niyomzima amesema amefanikiwa kusaini Yanga mkataba huo.

“Kweli nilifuatwa na timu nyingi sana na zilinipa ofa kubwa, moja ya timu ni kutoka Tunisia.
“Nyingine ni za hapa Tanzania, lakini nilikuwa nina mipango yangu na nimeamua kusaini,” alisema Niyonzima raia wa Rwanda.

Kuna taarifa Yanga itamtambulisha Niyonzima leo kwenye makao makuu ya klabu hiyo.
Kwa hisani ya Salehjembe blog

No comments:

Post a Comment