Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, May 13, 2013

BRANDT AANZA TAMBO BAADA YA KUFIKA ZANZIBAR



KOCHA Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts amesema ubora wa Uwanja wa Gombani uliowekwa nyasi bandia utawapa matokeo mazuri katika mechi yao dhidi ya Simba.

Kutokana na mazoezi wanayofanya kwenye uwanja huo, ni wazi Simba imekwisha habari yake ambao watacheza Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Brandts alisema amevutiwa na miundombinu ya uwanja huo, hivyo itakuwa ni fursa kwa wachezaji wake kuhitimisha msimu wa ligi hiyo kwa kuibuka na ushindi. 

Brandts alisema ana matumaini makubwa Yanga itaibuka na ushindi, ili waweze kulinda heshima  baada ya kuchukua ubingwa wa ligi hiyo.
Alisema wamefurahi kuona timu yake ikifanya mazoezi katika uwanja ulio bora, kitu ambacho ataweza kuijenga timu yake vizuri kabla ya kukutana na watani wao wa jadi Simba.

Brandts alisema kazi iliyobaki ni kuhakikisha wachezaji wake anawapa mbinu mbalimbali zitakazoweza kuwapatia ushindi.
Yanga ilianza kufanya mazoezi kwenye uwanja huo juzi, baada ya kutua katika kisiwa hicho Ijumaa wiki iliyopita.

Uongozi wa klabu ya Yanga kwa kushirikiana na benchi la ufundi, uliamua kubadilisha mazingira ya kambi ambao walikuwa na mazoea ya kwenda Bagamoyo.
Wakati huo huo, Brandts alisema wachezaji wake wapo fiti kiakili, kifikra na morali ya hali ya juu kuelekea mechi hiyo.

No comments:

Post a Comment