Pages

Monday, May 27, 2013

ABAJALO YABANWA MBAVU NA KARIAKOO LINDI UWANJA WA KARUME DAR ES SALAAM

Mashabiki wa Kariakoo  ya Lindi

Mshambuliaji wa Kariakoo Lindi, Salum Abilah akijaribu kumtoka beki wa Abajalo, Jamal Machelanga kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa uliochezwa katika Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam jana
TIMU ya Abajalo ya Dar es Salaam jana ilishindwa kutumia Uwanja wa nyumbani baada ya kukubali kutoka sare ya mabao 2-2 na Kariakoo ya Lindi kwenye mchezo Ligi ya Mabingwa wa Mikoa, mchezo uliochezwa Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo wa raundi ya pili ulishuhudia Abajalo wakijipatia mabao yake kipindi cha kwanza kupitia kwa mshambuliaji Abubakar Hiza dakika ya 20 na kiungo Wazir Abdallah dakika ya 39, wakati Kariakoo Lindi wakishangaa nyasi bandia  na maghorofa yaliyozunguka Uwanja wa Karume.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko na kuanza kucheza mchezo wa tahadhari kwani kila timu ilianza kucheza kwa  kujihami.
Kariakoo Lindi ambayo ilikuwa na mashabiki wengi ilibadilika na kucheza soka la kujiamini na kufanikiwa kurudisha mabao yote kupitia kwa nahodha wao Hanafi Suleiman dakika ya 64 na mshambuliaji Salum Abilah dakika ya 69 kwa njia ya penalty baada ya beki wa Abajalo Rahim Abdallah kushika mpira eneo la penalti.
Baaada ya kusawazisha mabao hayo Kariakoo iliyokuwa imeambatana na uongozi wote wa chama cha soka (LIREFA) wakiongozwa na Mwenyekiti wake Francis Ndulane walionyesha kandanda safi.

Baada ya mchezo kocha wa Kariakoo Lindi, Nyamwase Rashid na kusema kuwa timu yake ilipoteza umakini kipindi cha kwanza na kuruhusu mabao hayo lakini baadae wachezaji walibadilika na kuweza kurudisha mabao yote jambo ambalo anaamini kwenye mchezo wa marudiano watafanya vizuri.

“Timu ilipoteza umakini mwanzoni ila kwa matokeo haya naamini tutasonga mbele kwani ugeni wa uwanja wa nyasi bandia ulitugharimu”, alisema Rashid 

                                          
Kwenye mchezo wa juzi Friends Rangers iliwafunga African Sports ya Tanga mabao 2-1 kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Chamazi.

Mabao Friends Rangers yalifungwa na Hatibu Kuduku dakika ya 23 na Joseph Mwakigara dakika ya 80 huku lile la African Sports likifungwa na Thabit Digola dakika ya 67

Ligi hii inaendelea tena mwishoni mwa wiki 

No comments:

Post a Comment