Pages

Sunday, April 21, 2013

YANGA HAIKAMATIKI, YAICHEZESHA JKT RUVU GWARIDE TAIFA, YABAKISHA POINTI MOJA KUTWAA UBINGWA

Golikipa wa JKT Ruvu  Shaban Dihile akiwa amedaka mpira ambao mshambuliaji wa Yanga Simon Msuva alikuwa anaukimbilia kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliochezwa uwanja wa Taifa leo

Golikipa Shaban Dihile wa JKT Ruvu akipangua mpirs uliopigwa na Jerryson Tegete
Damasi Makwaya wa JKT Ruvu akiondoa mpira kwenye eneo la hatari huku Simon Msuva akijaribu kumnyang'anya

Wachezaji wa Yanga wakishangilia kwa kumpongeza Simon Msuva baada ya kufunga bao la kwanza

Vibweka vya mashabiki wa Janwani wakiwa wamebeba kitu mfano wa Tv 


Shaban Dihile wa JKT Ruvuakidaka mpira kichwani mwa Mbuyu Twite wa Yanga


YANGA leo imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JKT Ruvu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kwa matokeo hayo Yanga imetimiza pointi 56 na sasa inahitaji pointi moja tu ili kutawazwa mabingwa baada ya kuwa Simba imeshautema rasmi.
Bao la kwanza lilifungwa na Simon Msuva baada ya kupokea mpira wa kurusha uliorushwa na Mbuyi Twite.

Kipindi cha pili, Yanga SC walirudi wakiwa wanadhamira ya kuongeza mabao zaidi na kufanikiwa kupata mabao mawili zaidi, yaliyofungwa na Hamisi Kiiza dakika ya 59 na Nizar Khalfan dakika ya 64.
Kiiza alifunga kwa kichwa akiunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na David Luhende, baada ya Nizar Khalfan kuchezewa rafu nje kidogo ya eneo la hatari.

Nizar yeye alifunga baada ya kuuwahi mpira uliogonga mwamba na kurudi baada ya Frank Domayo kuunganisha krosi ya Haruna Niyonzima.

Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’/Said Mohamed dk 86, Mbuyu Twite, David Luhende, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Frank Domayo, Haruna Niyonzima, Nizar Khalfan/Said Bahanuzi dk90, Hamisi Kiiza/Jerry Tegete dk82 na Simon Msuva.

JKT Ruvu; Shaaban Dihile, Hassan Kikutwa/Sostenes Manyasi dk77, Stanley Nkomola, Ramadhani Madenge, Damas Makwaya, Nashon Naftali, Amos Mgisa, Ally Mkanga/Charles Thadei dk78, Mussa Mgosi, Zahor Pazi na Haroun Adolph.


No comments:

Post a Comment