Pages

Sunday, April 7, 2013

SHIRIKISHO LA SOKA TANZANIA YATOA PONGEZI KWA WAANDISHI WALIOSHINDA TUZO ZA EJAT


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limewapongeza waandishi watatu wa habari za michezo kwa kushinda Tuzo ya Umahiri wa Uandishi wa Habari (EJAT) inayotolewa na Baraza la Habari Tanzania (MCT).

Waandishi hao walioshinda katika kategori ya michezo na utamaduni ni Abdul Mohammed wa The African kwa upande wa magazeti na Abdallah Majura wa redio ABM kwa upande wa redio.

TFF tunawapongeza kwa ushindi huo uliotokana na makala zao ambazo zina mchango katika maendeleo ya mpira wa miguu, lakini pia ni changamoto kwa waandishi wengine ambao hawakufanikiwa kushinda.

Vyombo vya habari vina nafasi kubwa katika ustawi wa michezo ukiwemo mpira wa miguu, kwani katika nchi nyingine vimefichua rushwa. Ni matarajio yetu kuwa vyombo vya habari nchini navyo vitakuwa mstari wa mbele katika kufichua na kupambana na rushwa katika mpira wa miguu.

No comments:

Post a Comment