Pages

Monday, April 1, 2013

SERENA WILIAMS ATWAA UBINGWA WA SONY OPEN 2013 BAADA YA KUMFUNGA MARIA SHARAPOVA


 Wapiga picha wa vyombo vya habari wakimpiga picha nyota wa tenisi raia wa Marekani, Serena Williams baada ya kutawazwa bingwa mpya wa michuano ya wazi ya Sony 'Sony Open 2013', ushindi uliokuja baada ya kumchapa Maria Sharapova wa Russia kwa 4-6 6-3 6-0 katika fainali iliyopigwa Miami, Marekani mchana wa leo Jumapili, Machi 31. (Picha zote kwa Hisani ya Gazeti la Daily Mail la Uingereza).
 Serena Williams wa Marekani (kulia), akiwa ameshikilia taji la Sony Open 2013, baada ya kumshinda Mrusi Maria Sharapova (kushoto) katika fainali ya michuano kwa wanawake iliyopigwa Jumapili mchana huko Miami, Marekani.
 Hapa Serena Williams akiwa ameshikilia taji la ubingwa wa Sony Open huko Miami Marekani.
 Hapa Serena Williams akirudisha mpira kwa mpinzani wake Maria Sharapova (hayuko pichani) wakati wa mechi ya fainali ya Sony Open huko Miami Marekani. 
Hapa Maria Sharapova akirudisha mpira kwa mpinzani wake Serena Williams (hayuko pichani), wakati wa mechi ya fainali ya Sony Open huko Miami Marekani.
Serena hapa akishangilia baada ya kumalizika kwa pambano la fainali Sony Open dhidi ya Mrusi Maria Sharapova na kutawazwa bingwa mpya wa michuano hiyo kwa wanawake.
 Hapa Serena Williams akiwa ameshikilia taji la ubingwa wa Sony Open huko Miami Marekani.

No comments:

Post a Comment