Pages

Tuesday, April 2, 2013

REGAN MBUTA KUZIKWA LEO KIMAMBA KILOSA MOROGORO

mshambuliaji wa timu ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ya Polisi Tabora, Regan Mbuta aliyefariki Machi 31 mwaka huu usiku kwa ajali ya pikipiki maeneo ya Ipuli  mjini Tabora anazikwa leo nyumbani kwao Kimamba Kilosa, mkoa Morogoro
Kwa mujibu wahabari znilizopata kupitia kwa kocha wake Mwinyimad Tambaza, amesema yupo Morogoro tayari kwa kutoa heshima zake za mwisho kwa mchezaji huyo ambaye alikuwa muhimu kwa timu yake ya Polisi Tabora na soka la Tanzania.
Msiba huo ni mkubwa kwa wadau wa mpira wa miguu kwani Mbuta alikuwa mmoja wa washambuliaji tegemeo wa Polisi Tabora, na bao lake la mwisho aliyoifungia timu ilikuwa kwenye mechi ya mwisho ya FDL msimu huu dhidi ya Pamba ya Mwanza iliyochezwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora. Hivyo mchango wake tutaukumbuka daima.
LENZI YA MICHEZO inatoa pole kwa familia ya marehemu Mbuta, TAREFA na klabu ya Polisi Tabora na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito. Mungu aiweke roho ya marehemu Mbuta mahali pema peponi. Amina

No comments:

Post a Comment