Pages

Tuesday, April 23, 2013

RED COAST YASHIKILIA MSIMAMO WA LIGI DARAJA LA PILI DAR ES SALAAM NI BAADA YA KUIFUNGA SHARIF STARS 3-1


TIMU ya Red coast ya Kinondoni juzi iliifunga Sharif Stars ya Ilala mabao 3-1 kwenye mchezo wa Ligi Daraja la pili mkoa wa Dar es Salaam uliochezwa Uwanja wa Airwing Ukonga.

Mchezo huo ambao ulikuwa wa ushindani ulishuhudia timu zote kwenda mapumziko bila kufungana kutoka na safu za Ulinzi za timu zote kuwa makini katika kulinda goli.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko na Red coast ikafanikiwa kupata bao la kuongoza dakika ya 55 lililofungwa na  Mwinyi Ally, Ramadahani Said aliongeza bao la pili dakika ya 78 na mwisho lilifungwa na Idrisa Pandu dakika ya 90.

Bao la Sharifu Stars lilifungwa na Hassan Kuka dakika ya 65 baada ya kuwazidi mbio walizni wa Red Coast wakidhani kuwa ameotea.

Kwenye michezo mingine iliyochezwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Friends Rangers waliifunga Boom bo 1-0 lililofunga naRashid Khalfan dakika ya 14.

Abajalo FC ilitoshana nguvu na Day Break bila kufungana kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Makurumla.

No comments:

Post a Comment