Pages

Monday, April 22, 2013

RAS INNO KUZINDUA BENDI MWEZI UJAO


 Ras Inno Nganyagwa akionesha tuzo ya Kili Music.
Ras Inno akifanya vitu vyake jukwaani katika moja ya matamasha yake. 

BENDI ya mwanamuziki wa reggae nchini, Ras Inno Nganyagwa imekamilika na anatarajia kuizinduliwaa rasmi mwezi ujao jijini Dar es Salaam.


Ras Inno ambaye ni mshindi wa tuzo nne za mwanamuziki bora wa reggae Tanzania, amesema bendi yake hiyo ina wanamuziki 11 na itazinduliwa katika hafla maalumu katika ukumbi utakaotangazwa hapo baadaye.
Pia amesema nia ya kuanzisha bendi hiyo ni aweze kufanya kazi zake za muziki katika ufanisi bora  kwani bendi ya kudumu na wanamuziki wa kudumu hujenga ‘patern’ ambayo ni sawa na wachezaji waliozoeana uwanjani.

“Bendi hulinda ladha ya nyimbo husikapia show haziwezikubadilika na inasaidia kuwa na  uhakika wa kufanya kazi njema nje ya nchi kwani huleta tija ya kudumu tofauti ukiwa solo, kazi huja kwa msimu kutokana na mazoea hapa nchini”, alisema

Amesema bendi hiyo ni mojawapo ya miradi iliyo chini ya usimamizi wa taasisi yake Raggae Production House ambayo ni mahsusi kwa kupromoti muziki wa reggae, kwa ushirikiano na wadau wengine miongoni mwa mitindo mingine kwa kuzingatia weledi

“Dhima ni kuufufua muziki wa reggae hapa nchinisi kwa kuwa umekufa bali kuna mazingira yanayoufanya uonekane kama haupo na mashabiki wana hamu kubwa nao.”
Pia amedhamiria kufanya taasisi yake na bendi iwe vyenye hadhi na naamini mwanzo huu wa mapinduzi utaungwa mkono na wadau wote wenye mapenzi mema.

No comments:

Post a Comment