Pages

Tuesday, April 16, 2013

PISTORIUS KUTOSHIRIKI LONDON MARATHON



MWANARIADHA mlemavu bingwa wa medali ya dhahabu ya paralimpiki, Oscar Pistorius ameenguliwa katika michuano ya riadha ya kiangazi itakayofanyika jijini London, Uingereza.

Pistorius mwenye umri wa miaka 26, yuko nje kwa dhamana baada ya kushitakiwa kumuua rafiki yake wa kike Reeva Steenkamp, lakini anaruhusiwa kushindana kabla ya kesi yake haijaanza kusikilizwa.
Michuano hiyo ya riadha ya London pia inajumuisha wanaridha walemavu lakini mwenyekiti wa wa Riadha nchini humo, Ed Warner amesema Pistorius hatashiriki mbio hizo.

Warner amesema hataki kuona mashindano hayo ya riadha ambayo yatafanyika Jumapili kushambuliwa na vyombo vya habari kwa kuruhusu Pistorius kushiriki. Amesema suala hilo halihusiana na kama Pistorius ana hatia ama la, ila ni ugumu wa jinsi ya kumpokea mwanariadha huyo ambaye kila mtu anafikra tofauti dhidi yake inaweza isiwe vizuri hata kwa usalama wake.

No comments:

Post a Comment