Pages

Sunday, April 21, 2013

MAZOEZI KUWANIA TAJI LA MISS SINZA 2013 KUANZA APRIL 26

Miss Sinza 2012 ambaye pia ni Miss Kinondoni na Miss Tanzania, Brigitte Alfred mara baada ya kushinda taji hilo mwaka jana. Mchakato wa kumsaka mrithi wa taji hilo utaanza April 26 kwenye ukumbi wa Meeda, Sinza.
Na Mwandishi Wetu
MAZOEZI ya warembo watakaowania taji la urembo la Sinza, Miss 2013 yataanza Aprili 26 kwenye ukumbi wa Meeda uliopo Sinza Mori na Lufungila jijini.
Taji la Miss Sinza linashikiliwa na Miss Tanzania, Brigitte Alfred ambaye ataiwakilisha Tanzania katika mashindano ya urembo ya dunia, Miss World 2013 mwezi Agosti mwaka huu.
Mratibu wa mashindano hayo, Majuto Omary alisema kuwa maandalizi ya mazoezi hayo yamekamilika na yatasimiwa na kamati ya maandalizi huku ikitafuta mwalimu kwa ajili ya kuwanoa.
Majuto alisema kuwa warembo waliowahi kushiriki mashindano hayo wanaruhusiwa kuja kutoa sapoti kwa warembo wapya na kamati yao itawapa nafasi ya kuwafundisha warembo wapya ili kuwapa ‘mbinu’ mbali mbali za mashindano hayo.
Alisema kuwa fomu za kuomba kushiriki katika mashindano hayo zinapatikana kuanzia leo (Ijumaa) maduka ya Zizzou, Sinza Afrika Sana, Meeda, Ofisi za Miss Tanzania, Ofisi za gazeti la Mwananchi (Tabata) au kwa njia ya mitandao (blogs), balilemajuto, sufiani mafoto, saluti5 au kutuma kwa njia ya email,majutoy2k@yahoo.co.uk
“ Lengo letu kubwa ni kumsaka mrithi taji la Miss Tanzania, Miss Kinondoni na Sinza, mataji yote hayo yapo katika kituo chetu, tumejipanga kulinda heshima yetu na tunaamini titafanikiwa kwa heshima ya wakazi wa Sinza, Kinondoni na Tanzania kwa ujumla,” alisema Majuto.

Alisema kuwa wanawakaribisha warembo wanaotaka ‘kupata taji’ kuchukua fomu zao ambazo zinatolewa bure. Majuto pia aliwaomba wadhamini wanaotaka kujitangaza kupitia mashindano yao wanaruhusiwa kuja kudhamini mashindano hayo na milango ipo wazi
.

No comments:

Post a Comment