Pages

Monday, April 1, 2013

MANCHESTER YAFUNGWA NYUMBANI NA CHELSEA,, SASA CHELSEA KUCHEZA NUSU FAINALI NA MANCHESTER CITY



Chelsea imeichapa Manchester United  bao 1-0 katika mechi ya robo fainali ya Kombe la FA iliyochezwa kwenye Uwanja wa Stamford Bridge jijini London, leo.

Bao la Chelsea lilifungwa na  Demba Ba dakika ya 49, baaada ya kuunganisha pasi ya juu ya Juan Mata. Mchezo wa nusu fainali hiyo, Chelsea itavaana na jirani wa Manchester United, Manchester City.


Kwa ushindi huo, Chelsea imesonga hadi nusu fainali ya kombe la FA huku ikiondoa matumaini ya Man United kuendelea kuwemo katika kuwania kombe hilo lenye heshima England.

Mechi ya kwanza iliyopigwa mjini Manchester, timu hizo zilimaliza dakika 90 kwa sare ya mabao 2-2, hivyo kila timu ulitaka ushindi lakini wageni Chelsea waliocheza vizuri na kumiliki mpira leo.

Chelsea walipoteza nafasi nyingi za kufunga kupitia Mata, Oscar, Ba na Hazzard wakati Man United walipata nafasi chache kupitia Chicharito na van Persie lakini hawakuzitumia au ziliokolewa.



No comments:

Post a Comment