Pages

Tuesday, April 23, 2013

MWAMUZI MARK CLATTENBURG ARUDI TENA DARAJANI CHELSEA!!


REFA Mark Clattenburg atarudi Stamford Bridge kuichezesha Chelsea kwa mara ya kwanza tangu asafishwe sakata la Ubaguzi dhidi ya John Obi Mikel na huko Emirates, Arsenal imeamua kukata Rufaa kupinga Kadi Nyekundu ya Straika wao Olivier Giroud.
JUMAPILI, Refa Mark Clattenburg atarudi Uwanja wa Stamford Bridge kuichezesha Chelsea kwa mara ya kwanza baada ya Miezi 6 baada ya kusafishwa kutumia Ubaguzi dhidi ya Kiungo wa Chelsea John Obi Mikel.

Chelsea walilalamika kuwa Clattenburg alitumia lugha isiyofaa dhidi ya Mikel wakati wanachapwa Bao 3-2 na Manchester United Mwezi Oktoba Mwaka jana Uwanjani Stamford Bridge.

Baada ya uchunguzi wa FA, Refa huyo, ambaye alitamka jambo hilo limemtisha, Clattenburg alisafishwa kuhusu tuhuma zote.

Baadaye Klabu ya Chelsea ilitoa tamko la kusikitika kuhusu walivyochukulia suala hilo na kutaka radhi na sasa, Miezi 6 baadae, Clattenburg ataichezesha Chelsea watakapocheza na Swansea City kwenye Mechi ya Ligi.

No comments:

Post a Comment