Pages

Saturday, April 27, 2013

JESHI STARS WANAWAKE YATWAA UBINGWA WA MASHINDANO YA WAVU YA MAADHIMIASHO YA MUUNGANO

Wachezaji wa Jeshi Stars wakishangilia ushindi na familia zao

Nahodha wa Jeshi Stars akikabidhiwa kikombe cha ubingwa wa mashindano ya muungano na  Naibu Mkurugenzi wa Michezo wa Wizara ya Habari, Vijana, Michezo na  Utamaduni, Juliana Yassoda

Nahodha wa Magereza akipokea kikombe cha mshindi wa pili toka kwa Naibu Mkurugenzi wa Michezo wa Wizara ya Habari, Vijana, Michezo na  Utamaduni, Juliana Yassoda

Mchezaji wa Magereza akirudisha mpira kwa wapinzani wao Jeshi Stars

Wachezaji wakipeana fair play baada ya mchezo kumalizika

Magereza stars

Jeshi Stars

TIMU ya Jeshi Stars wanawake jana walifanikiwa kutwaa kombe la Muungano baada ya kuifunga Magereza seti 3 kwa 0  kwenye mchezo wa wavu uliochezwa Uwanja wa ndani wa Taifa.

Mchezo huo ulikuwa wa upande mmoja ulishuhudia kila seti Jeshi wakimaliza wakiongoza.
Jeshi walishinda kwa 25 kwa 20, 25 kwa 17 na 25 kwa 19 na kujichukulia kombe la Muungano kirahisi.

Zawadi ya mchezaji bora ilikwenda kwa Christina Msuya na Yasinta Remmy wa Jeshi Stars na kupewa zawadi ya mpira mmoja mmoja na Hellen Mwegoha  wa Magereza ambaye na pia alipewa mpira.

No comments:

Post a Comment