Pages

Friday, April 5, 2013

CHELSEA YAIUA RUBIN KAZAN 3-1, BENFICA YAILAZA NEWCASTLE 3-1, TOTTENHAM YABANWA MBAVU NA BASEL 2-2 HUKU FENERBAHCE IKIIVURUMISHA LAZIO 2-0 KWENYE EUROPA LEAGUE


KLABU TATU za England, Chelsea, Tottenham na Newcastle, jana, Aprili 4 zikiwa dimbani kucheza Mechi za kwanza za Robo Fainali huku Chelsea na Tottenham wakianzia Nyumbani na Newcastle kucheza ugenini. Chelsea wameibuka na ushindi wa bao 3-1 dhidi ya Rubin Kazan. 

Chelsea ndiyo waliotangulia kupata bao dakika ya 16 kupitia kwa mchezaji wao Fernando Torres Baadaye mchezaji wao Victor Moses akaongeza tena dakika ya 32 na kufanya 2-0 dhidi ya Rubin Kazan. Dakika ya 41 mchezaji wa Rubin Kazan Bebars Natcho akaipatia bao kupitia mkwaju wa Penati baada ya John Terry kuunawa mkwaju eneo la penati, Dakika ya 70 Fernando Torres akaiongezea bao Chelsea baada ya kufunga kwa kichwa baada ya kutumiwa pasi safi ya juu.
Gylfi Sigurdsson akiwafungia bao Spurs katika dakika ya 58 kipindi cha pili.
Wao Benfica wameichapa Newcastle bao 3-1 bao zilizofungwa kipindi cha kwanza na chapili kupitia kwa Rodrigo dakika ya 25' na Lima akifunga bao la pili katika dakika ya 65' na Óscar Cardozo akimaliza la tatu kwa mkwaju wa penati dakika ya 71' huku Papiss Demba Cisse akifunga bao la kufutia machozi na akianza kuwafungia Newcastle dakika ya 12.

Ogenyi Onazi akifanya ndivyo sivyo hapa na huku akiwa na kadi ya njano na hiki kimesababisha atolewe kwa kadi nyekundu hapa
Kipa wa Chelsea Petr Cech akiruka kupangua mpira na huku David Luiz akiunyemelea mpira huo

Mchezaji Emmanuel Adebayor akifunga goli la kwanza dakika ya 40 Fabian Frei akitupia kwa kichwa dakika ya 35

Victor Moses akitupia bao la pili hapa

Rodrigoakishangilia baada ya kusawazisha.

Fernando Torres kwenye patashika na mchezaji wa Rubin Kazan

Fernando Torres akishangilia baada ya kazi nzuri

Papiss Cisse akifunga bao la pekee dakika ya 12
Papiss Cisse akishangilia.

Mchezaji wa Fenerbahce Pierre Webo (kushoto) akimenyana na mchezaji wa Lazio Hernanes
Mchezaji wa Tottenham Lewis Holtby akichuana na Mohamed Salah usiku

No comments:

Post a Comment