Pages

Saturday, April 27, 2013

ASNATH KUTOKA CHUO KIKUU MZUMBE ATWAA TAJI LA REDD'S MISS HIGHER LEARNING MOROGORO 2013


Mshindi wa Shindano la Redd’s Miss Higher Learning Mkoa wa Morogoro, Anitha Mwakitwange kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe akipunga mkono mara baada ya kuvikwa taji hilo usiku wa kuamkia jana katika shindano lililofanyika Mjini Morogoro. Anitha aliwashinda warembo wenzake 10 aliokuwa akiwania nao taji hilo.
 
Redd’s Miss Higher Learning Mkoa wa Morogoro, Anitha Mwakitwange(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili Rosemary Aloyce (kulia) na Mshindi wa Tatu Tarchisic Mtui mara baada ya warembo hao kutawazwa kuwa ndio washindi wa Shindano hilo usiku wa kuamkia jana katika shindano lililofanyika Mjini Morogoro. Anitha ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe aliwashinda warembo wenzake 10 aliokuwa akiwania nao taji hilo.

 Majaji wa shindano hilo wakiwa tayari katika meza yao kusubiri washiriki wa Redd's Miss Higher Learning Morogoro kupanda jukwaani kuwania taji hilo.
 Mashabiki na wapenzi wa Sanaa ya Urembo kutoka Mkoa wa Morogoro na wengi wao wakiwa ni wanafunzi kutoka Vyuo vya Mzumbe, SUA, Jordan, St Joseph na MSJ wakisubiri kuanza kwa shindano hilo la Redd's Miss Higher Learning 2013.

Washiriki wa shindano la  Redd’s Miss Higher Learning Mkoa wa Morogoro wakicheza show ya ufunguzi wa shindano hilo lilifanyika usiku wa kuamkia jana na kushirikisha warembo 11 kutoka vyuo mbalimbali vya elimu ya Juu mkoani humo.
 Mwakilishi wa Kamati ya Miss Tanzania ambaye ni Afisa Habari wa Kamati hiyo, Hidan Rico akizungumza machache.
 Huyu alibuni vazi lake kwa Kitenge na makaratasi.
 Huyu alitumia Majani ya mti wa Muashock...
 Kiroba nacho kilichukua nafasi yake kwa mrembo huyu ....
 Miss Higher Learning yeye aliamua kutumia majani ya maua kutengeneza kauni lake maridani la ubunifu.
 Wapenzi wa sanaa ya urembo wakifuatilia kwa umakini onesho hilo.
 Msanii chipukizi wa Mkoa wa Morogoro, ambaye ni mwanafunzi wa Chuo cha St Joseph ajulikanae kama Jose alitumbuiza..
 Ulifika wasaa wa kivazi cha Ufukweni na kila mmoja alienda Mindu kuogelea kwa kivazi chake...
 Huyu aliingia hivi katika maji...
 Huyu alivaa hivi...
 Ilikuwa ni raha kwa mashabiki usiku huo ndani ya Savoy mjini Morogoro...
 Miss Tanzania namba Eugenia mbili nae alikuwepo kushuhudia shindano hilo
 Ilikuwa ni shangwe kwa wapenzi na mashabiki wa sanaa ya urembo Morogoro hasa meza hii ya Mzumbe ambayo ilishajua wazi kuwa taji ni lao mapemaaa...
 Vazi la usiku lilipita na kisha tano bora ikatangazwa...

Warembo waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora ya Redd’s Miss Higher Learning Mkoa wa Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja maara baada ya kutwajwa wakati wa shindano hilo lilifanyika usiku wa kuamkia jana na kushirikisha warembo 11 kutoka vyuo mbalimbali vya elimu ya Juu mkoani humo. Kutoka kushoto ni Tarchisic Mtui, Rosmary Aloyce,Hellen Mhando, Tausi Idd na Asnath Mwakitwange.  
 Washiriki wote ndio hawa hapa...
 Mzee wa Magube Gube!! Barnaba Boy aliwapagawisha vilivyo wapenzi wa sanaa ya urembo hasa wanafunzi hawa kutoka vyuo mbalimbali vya Elimu ya Juu Mkoani Morogoro.  
Walijiachia vilivyoo...katika sho hiyo kali 
KWA HISANI YA FATHER KIDEVU BLOG

No comments:

Post a Comment