Pages

Saturday, March 30, 2013

WACHEZAJI WATATU WAFA KWA AJALI


WACHEZAJI watatu wa klabu ya DC Motema pembe-DCMP ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC wamefariki dunia kwa ajali ya gari iliyotokea jijini Kinshasa jana. Wachezaji hao ambao ni golikipa Guelor Dibulana, washambuliaji Hugues Muyenge na Mozart Mwanza walikuwa wakirejea kutoka katika maombi katika kanisa la Saint- Dominique lililopo Kinshasa ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya sikukuu ya Pasaka ambapo gari lao liligongwa na lori. Kwa mujibu wa taarifa za hospitali mchezaji mwenzao Mbindi ambaye alikuwa akiendesha gari hilo alisalimika pamoja na abiria mwingine lakini wote walipata majeraha makubwa. DCMP ilitarajiwa kupambana na AS Vita Club siku ya Jumapili ya Pasaka na haijajulikana kama ratiba hiyo itaahirishwa kutokana na tukio hilo la kuhuzunisha lililotokea.

No comments:

Post a Comment