Pages

Friday, March 29, 2013

VICTOR ANICHEBE WA EVERTON APELEKA ZAWADI WODI YA WATOTO KATIKA HOSPITALI YA WHISTON.


Delighted: Everton striker Victor Anichebe poses with children at Whiston Hospital
Mshambuliaji wa Everton Victor Anichebe akiwa katika picha na watoto katika hospitali ya Whiston.
Mshambuliaji wa Everton Victor Anichebe amefanya matembezi ya ghafla yaani'Surprise visit' kwa kutembelea wodi ya watoto katika hospitali ya Whiston akiwa na zawadi maalumu ya sikukuu ya Pasaka 'Easter eggs'.

Anichebe mwenye umri wa miaka 24, amefanya matembezi hayo baada ya mazoezi hapo jana, ambapo alipiga picha na watoto waliokuwemo ndani ya wodi hiyo ambao walikuwa wenye furaha ambapo mbali ya kuzungumza nao pamoja na familia zao pia alijumuika nao katika michezo.

Anichebe amenukuliwa akiongea na televisheni ya Everton akisema 
 'Nadhani ni jambo kubwa kwenda sehemu kama hii na kukutana na nyuso za watoto zenye furaha, siku zote hili ni kubwa'

Surprise visit: Anichebe came to the hospital with Easter eggs and also took part in games
Ziara ya ghafla: Anichebe akiwa na  zawadi ya Pasaka ambapo alishiriki michezo.

'Nimefurahi sana kuwaona wakiwa na furaha, itachukua tena muda mrefu kukutana na watoto tena kama hivi. Nitakuwa na mtoto mmoja au wawili watakuja nyumbani, na nimefanikiwa kuwapa tabasamu katika nyuso zao na licha ya kwamba kuna mmoja au wawili wengine walikuwa wanalia lakini watakuwa nyumbani siku ya Pasaka'

Anichebe aliwakabidhi mayai ya zawaida watoto hao waliokuwa na amani ya moyo wakati huo wa ziara yake hiyo ambao aliingia wodi tatu tofauti na kuungana na wafanyakazi wa wodi hizo.

'Kulikuwa na baadhi ya mashabiki wa Everton na wengine wa  Liverpool na Manchester United pia , lakini hilo si tatizo kujua nani shabiki wa Everton, kikubwa ni kuja kuwaona watoto na kuwasapoti'
On form: Anichebe is on course to score ten goals for the first time in his career, he currently has seven 
Katika kiwando: Anichebe akifumua shuti kufunga goli.

Kwasasa mshambuliaji huyo ana furahia msimu akiwa na Everton na ana matumaini kuwa atakuwa na msimu mzuri zaidi wa kufunga magoli mengi kwa mara ya kwanza.

Ana jumla ya magoli saba na endapo meneja wake David Moyes atampa nafasi katika mchezo wa jumamosi dhidi ya Stoke, Anichebe atakuwa anafikisha jumla ya michezo 50 katika kikosi cha kwanza.
Half-century: If manager David Moyes (pictured) starts Anichebe on Saturday against Stoke, it wi;; be his 50th career league start 
Meneja wa Everton David Moyes (katika picha)

No comments:

Post a Comment