Pages

Sunday, March 31, 2013

MANCHESTER UNITED KUMSAJILI ALCANTARA WA BARCELONA KUFUATIA BABA YAKE KUSEMA......

Wanted: Barcelona's Thiago Alcantara is a target for Manchester United
Thiago Alcantara aliyesimama ambaye kwasasa yuko katika mawindo ya United.

Manchester United wanatarajiwa kuanza tena pilika za kumtaka kiungo wa Barcelona Thiago Alcantara kufuatia baba yake mzazi na mshambuliaji huyo kuweka wazi kuwa kijana wake yuko tayari kuihama klabu Barcelona.
 
United imekuwa katika mawindo ya kumchukua kiungo huyo kwa zaidi ya miaka mitatu ambapo miezi 18 iliyopita ofa ya pauni milioni 15 ilikataliwa na Barca.
 
kiungo huyo mwenye umri wa miaka 21 alikuwa akijitutumua kutaka kujiimarisha katika kikosi cha kwanza lakini baada ya mambo kwenda tofauti sasa amekubali kuondoka ndani ya klabu hiyo.
 
Amenukuliwa baba yake Mazinho akisema 
 ‘Kijana wangu atacheza sana katika timu nyingine duniani, anajifunza mengi katika soka kutoka kwa wachezaji wakubwa na kwasasa Thiago anataka kucheza mpira. 

‘Hakuna anayejua nini kitatokea baadaye, mpira wa miguu una mambo mengi na lolote linaweza kutokea . Kama Thiago atakuwa anataka kucheza kombe la dunia 2014 anapaswa kupata nafasi ya kucheza sana.
‘Thiago ana ubora wa mafanikio ndani ya Barca'

‘Si dhani kama Barca itanunua wachezaji wakati wa kiangazi, wana wachezaji wengi ambao wanaweza kucheza nafasi ya kiungo. Pia kaka yake Rafinha atakuwa ni sehemu ya wachezaji wa kikosi cha kwanza msimu ujao’
Big fan: Sir Alex Ferguson will look to bolster his midfield in the summer
Sir Alex Ferguson anasema wanahitaji kuipa nguvu sehemu ya kiungo wakati wa kiangazi.

Alcantara alielekea nchini Hispania wakati akiwa na umri wa miaka mitano na alijiunga na Barcelona miaka tisa baadaye.

Aliaanza kuichezea Barca kwa mara ya kwanza katika mchezo ambao Barca ilikabiliana na Mallorca mwaka 2009, lakini akiifungia goli la kwanza mwaka uliofuata.
Aliingia mkataba mpya miaka miwili iliyopita mkataba wenye thamani ya EURO milioni (£25m).
Competition: Alcantara has been unable to force his way into the side

No comments:

Post a Comment