KATIBU
Mkuu wa zamani wa kilichokuwa Chama Cha Soka nchini (FAT) (TFF), Michael
Wambura, anatarajia kutoa tamko lake leo saa sita kamili za mchana, katika
Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo juu ya kuenguliwa kwake kugombea nafasi ya
Makamu wa Rais wa Shirikisho hilo, katika Uchaguzi uliopangwa kufanyika Februari
24.
Wambura
ameendelea kung’ang’aniwa na wadau wa soka, kwa kumtoa kila anapojaribu kuwania
nafasi yoyote katika medani ya mpira wa miguu hapa nchini, ikiwapo
TFF.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam, Wambura alisema kwamba anatafakari pamoja na kupokea
barua kutoka TFF juu ya kumuengua kwake kuwania nafasi ya Makamu wa
Rais.
Alisema
anaitumia nafasi hiyo kukaa na kupitia vifungu mbalimbali vilivyokuwa kwenye
Kanuni za TFF, kabla ya kuzungumzia mustakabali wa soka la hapa
nchini.
“Sijataka
kukurupuka kutoa uamuzi baada ya kusikia kwenye vyombo vya habari kuwa rufaa
yangu haijakuwa nzuri baada ya matokeo yale yale ya Kamati ya Uchaguzi
kujirudia.
“Naamini
nipo tayari leo mchana kuzungumzia yote kwa nia ya kutoa picha kamili ya matokeo
ya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa TFF utakaofanyika Februari 24,”
alisema.
Katika
Uchaguzi huo, nafasi pekee ya Urais imebaki kwa mgombea wake, Athumani Nyamlani,
baada ya mpinzani wake, Jamal Malinzi naye kutupwa na Kamati ya Rufaa kwa madai
hana uzoefu.
No comments:
Post a Comment