Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, February 14, 2013

BASI LA TAIFA STARS HADHARANI

Hatimaye basi la Timu ya Taifa, Taifa Stars lililokuwa likisubiriwa kwa hamu sasa limewasili na liko tayari kukabidhiwa na Bia yako ya Kilimanjaro Premium Lager kwa Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF) ili Taifa Stars iweze kulitumia.
 Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, inayodhamini Taifa Stars, George Kavishe alisema hii ni katika malengo yao ya kuinua hadhi ya timu ya Taifa ambayo kwa sasa imeonesha kiwango cha hali ya juu.
Alisema basi hilo aina ya Yutong lenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 200, ni kubwa na la kisasa kabisa lenye uwezo wa kubeba abiria 50 pamoja na dereva na kuwa lina nafasi kubwa kutoka kiti kimoja hadi kingine hivi kuwafanya wachezaji wakae kwa raha zaidi wanaposafiri, basi hili linatarajiwa kukabidhiwa kwa Taifa Stars Februari 21 katika hafla itakayofanyika katika makao makuu ya TBL Ilala Jijini Dar es Salaam na itahudhuriwa na wadau mbalimbali wa soka nchini na wageni wengine.
Bia ya Kilimanjaro Premium Lager ilianza kuidhamini Timu ya Taifa tangu mwezi Mei mwaka jana kwa kuwekeza zaidi ya bilioni mbili kwa mwaka kwenye timu hii kwa muda wa miaka mitano.Udhamini wa Kilimanajro Premium Lager ndio mkubwa kabisa ambao TFF imewahi kupokea kutoka kwa kampuni au shirika lolote nchini kudhamini mpira

No comments:

Post a Comment