Wachezaji
wa simba, wakimpongeza kiungo wao Mwinyi Kazimoto, baada ya kuifungia
timu yake bao, wakati wa mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Sheikh
Amri Abeid, Jijini Arusha jana.
*************************************
TIMU
ya Simba ya jijini Dar es Salaam, jana ilivutwa shati na JKT
Oljoro baada ya kufungana bao 1-1, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara, mzunguko wa pili uliochezwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri
Abeid jijini Arusha.
Kwa
timu ya Simba imetimiza sare ya pili tangu kuanza kwa mzunguko wa
pili wa ligi hiyo, baada ya wiki iliyopita kulazimishwa sare kama hiyo
na JKT Ruvu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuifanya
Simba kutimiza jumla ya pointi
28, baada ya kucheza mechi 16, huku watani wao Yanga wakiongoza kwa kuwa
na pointi 33 na mchezo mmoja mkononi, wakati Azam FC ya pili wakiwa na
pointi 30 na mchezo mmoja mkononi.
Bao la JKT Oljoro, lilifungwa na Paul Nonga, katika dakika ya tisa tu tangu kuanza kipindi cha pili.
No comments:
Post a Comment