Pages

Tuesday, February 19, 2013

RAIS TENGA ABARIKI MAAMUZI YA KAMATI YA MTINGINJOLA YA KUTUPA REVIEW


Rais wa shirikisho la soka nchinji
 
Leordigar Chilla Tenga amesema kuwa alishauriwa visivyo juu ya kuwepo fursa ya maombi ya mapitio ya maamuzi ya kamati ya Rufaa ya uchaguzi kwa wagombea walioenguliwa na kamati hiyo.

 
Tenga ametoa kauli hiyo kwenye mkutano wake na waandishi wa habari mchana wa leo ambapo amesema chama cha mpira kiliunda vyombo vyake vya kimaamuzi kwa taratibu na kwamba maamuzi ya vyombo hivyo yanapaswa kuheshimiwa.
 
Amesema ni kweli alitamka kuwa wagomboea walioenguliwa katika kinyanganyoro hicho cha uchaguzi kufuata taratibu ambapo alieleza waandishi wa habari juu ya fursa tatu za mwisho kupitia baada ya maamuzi ya kamati ya rufaa ya uchaguzi ya Iddi Mtinginjola kumalizika.
Amesema hatua ya kwanza aliyopendekeza ilikuwa review, kwenda fifa na ikishindikina basi ni kwenda CAS.
Amesema kuwa TFF haina tatizo na maamuzi ya kamati ya rufaa ya uchaguzi kwa kuwa jambo hilo limepitia katika mikono ya sheria na kwamba inawezekana kukajitokeza mitazamo tofauti ya tafsiri ya kisheria, hivyo wanaheshimi maamuzi ya chombo hicho ambacho kimeundwa kwa kufuata utaratibu.
Rais Tenga amesema kwa vile hicho ndicho chombo cha mwisho nchini katika masuala ya uchaguzi alishauriwa kuwa kingeweza kufanya review.
 
“Kwa vile hakuna chombo kingine, nikashauriwa kuwa kinaweza kufanya review. Katika utaratibu wa kutoa haki, uamuzi ni lazima uwe wa wazi kwa kutoa sababu. Nilidhani hilo linawezekana, kwani Mahakama Kuu hufanya hivyo. Kwa hili uamuzi wa Mtiginjola ni sahihi,” amesema Rais Tenga.
Kamati ya Mtiginjola iliyokutana jana (Februari 18 mwaka huu) ilitupa maombi ya review yaliyowasilishwa mbele yake na waombaji uongozi watano kwa vile hakuna kipengele chochote kwenye Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi kinachotoa fursa hiyo.
 
Waombaji hao walikuwa Jamal Emil Malinzi aliyeenguliwa kugombea urais wa TFF na Hamad Yahya aliyeondolewa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania uenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board).
 
Wengine ni walioomba kuwania ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF na Kanda zao kwenye mabano; Eliud Peter Mvella (Iringa na Mbeya), Farid Salim Nahdi (Morogoro na Pwani) na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu).


No comments:

Post a Comment