Pages

Wednesday, February 13, 2013

NAIBU WAZIRI WA HABARI, MICHEZO, UTAMADUNI NA VIJANA AMAS MAKALA APINGA JAMAL MALINZI KUENGULIWA KWENYE KINYANG'ANYIRO CHA URAIS WA TFF

Wakati wadau mbalimbali wakiendelea kujitokeza katika vyombo mbalimbali vya habari wakionyesha kutoridhishwa kwao na wakipinga waziwazi maamuzi ya kamati ya rufaa ya uchaguzi ya shirikisho la soka nchini TFF ya kumuengua aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Rais wa shirikisho la soka nchini Jamali Emily Malinzi, naye naibu waziri wa habari utamaduni na michezo Amos Makala amejitokeza kupinga maamuzi hayo akisema haki haikutendeka.
 
Akiongea moja kwa moja katika kipindi cha michezo cha Sports Extra cha Clouds FM akiwa jimboni kwake mheshimiwa Makalla amesema maamuzi ya kamati rufaa ya uchaguzi iliyo chini ya Iddi Mtingijola yamemshitua sana hasa kutokana na sababu zilizo elezwa hususani juu ya sifa ya uzoefu wa miaka 5.
Makalla amesema maamuzi ya kamati hiyo yana ashiria kutaka kuwandosha watanzania katika mapenzi yao katika soka kama ambavyo imekuwa ikionekana katika siku za hivi karibu ambapo Tanzania imeanza kujenga upya mpira wa miguu na tayari timu ya taifa ikianza kupata matokeo mazuri dhidi ya vigogo wa soka barani Afrika kama Zambia na Cameroon.
 
Naibu waziri huyo akizungumza kama mdau wa michezo nchini huku akijinasibu kuwa yeye bado ni mchezaji akiwa nahodha wa timu ya bunge la jamhuri ya muungano, amemtaka Rais wa TFF Leordigar Tenga kuaangalia upya juu ya maamuzi ya kamati yake yasije yakawatoa watanzania katika mapenzi ya soka wakati huu ambapo Rais wa nchi Jakaya Mrisho Kikwete amekuwa akijitahidi kuhakikisha michezo inakuwa nchini.
Jana kamati ya rufaa ya uchaguzi ya TFF ilitangaza kumuondoa Jamali Malinzi katika kinyanyiro cha kuwania uongozi ndani ya shirikisho hilo kwa nafasi ya Rais kutoka na kukosa sifa ya uzoefu wa uongozi wa michezo kwa kipindi cha miaka 5 mfululizo, baada ya kukatiwa rufaa na mdau mmoja wa michezo aliyejulikana kwa jina la Agape Fue.
 
Agape pia ndani ya rufaa yake alihoji juu ya sifa ya uadilifu wa Malinzi akitumia kigezo cha mgombea huyo kupinga waraka wa TFF wa zoezi kupiga kura mabadiliko ya katiba ukiwa ni mwongozo wa moja kwa moja kutoka FIFA ambao walimtaka mwanachama wake kufanya mabadiliko ya katiba yake kwa kuingiza kipengele cha kuundwa vyombo mbalimbali kama ilivyokuwa kamati ya rufaa ya uchaguzi, jambo ambalo hapo kabla Jamali Malinzi alilipinga.

Malinzi ameenguliwa kwa kukosa sifa kupitia vifungu vya katiba sehemu ya uchaguzi ibara 9(3) kifungu namba 29, 39(3) na 12(b)(d) hivyo rufaa dhidi yake iliyokatwa na Agape Fueyake imeshinda.

No comments:

Post a Comment