Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limesitisha ukamishna wa Hafidh Ali. Uamuzi huo umefanywa na Kamati ya Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika iliyokutana Januari 17 mwaka huu jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa barua ya Katibu Mkuu wa CAF, Hicham El Amrani kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), ukamishna huo umesitishwa kwa vile hadi sasa Shirikisho hilo halijapata ripoti ya mechi namba 78 kati ya Comoro na Libya ambayo Ali aliteuliwa kuisimamia.
Hivyo, ukamishna wa Ali umesitishwa hadi hapo CAF itakapopokea ripoti kuhusiana na mechi hiyo ambayo ilikuwa ni kutafuta tiketi ya kucheza Fainali za AFCON zilizofanyika mwaka huu nchini Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment