Pages

Saturday, February 23, 2013

MANCHERSTER UNITED YAIFUNGA QPR 2-0

Manchester United leo wakicheza ugenini Uwanja wa Loftus Road wameifunga Timu ya QPR Bao 2-0 na kuongeza alama zaidi kufika 15 mbele ya Mabingwa watetezi Manchester City ambao wapo nafasi ya pili na ambao kesho Jumapili wanaikaribisha Chelsea Etihad ambao wako nafasi ya 3 ambao wanapointi 49 nyuma ya City wenye pointi 53. Kesho kama City watafungwa na Chelsea watawakalia vibaya mabingwa hao.


Goli la kwanza limefungwa na Rafael Da Silva dakika ya 23 baada ya kuachia shuti kali na la mbali.
Goli la pili limefungwa na mkongwe Ryan Giggs dakika ya 80 baada ya kukatiza kwa mabeki wa QPR na kuwaduwaza kubaki wakiduwaa wakidhani ni offside kumbe ndivyo sivyo.Mechi hii pia imemsababishia majeraha mchezaji wao RVP kipindi cha kwanza na kulazimika kutoka na nafasi yake akaichukuwa Welbeck dakika ya 41. Kocha mkuu wa England Roy Hodgson alikuwepo kushuhudia mtanange huo uliochapwa jioni hii saa 12.00 na kujionea vijana wake wakiparangana na timu hiyo ya mkiani mwa ligi hiyo ya EPL yenye watazamaji wengi Duniani. Ryan Giggs na Esteban Granero wa QPR wakichuana vikali leo Harry Redknapp, manager wa Queens Park Ranger leo alikuwa amepania sana kufunga lakini Vijana wake wakakutana na kisiki cha Fergie wakamwangusha na hatimaye kuendelea kushikilia mkia huo wa EPL. Manager Sir Alex Ferguson akifatilia vijana wake wakitafuta pointi 3 muhimu ugenini.Michael Carrick akichuana na mchezaji wa QPR Adel Taarabt Hakunaga: Rafael kufunga goli la kiwango ...kiasi kile Rafael akishangilia na wenzake baada ya kufunga goli la kwanza na la kiwango dakika ya 23Meneja wa England Roy Hodgson akifatilia mtanange huo kwa makini
Pain game: Robin van Persie collides with a cameraman
Robin van Persie akijiugulia maumivu chini
Concern: Robin van Persie receives treatment on the touchline after picking up an injury
Robin van Persie ... daktari bora utoke si ndyo.. au utaendelea..Angalia...kama vipi we toka usije umia zaidi...
Ouch! Van Persie receives medical treatment after his collision
Van Persie akipata matibabu ya haraka baada ya kuumia
Robin van Persie akipumzika baada ya kupata majeraha mapema kipindi cha kwanza na Kocha Alex Ferguson kumtoa haraka kupumzika mapema kwa ajili ya mechi zijazo.Ushindi ni muhimu: Harry Redknapp, meneja wa Queens Park Ranger na kulia ni Sir Alex Ferguson leo kila timu ilihitaji ushindi. QPR wapo mkiani wanataka kujinasua, United wapo juu wanataka kukwea zaidi.Ryan Giggs akishangilia na kulia ni Wayne Rooney baada ya kuifunga goli la 2 Queens Park Rangers Loftus Road leo February 23, 2013
VIKOSI:
QPR: Julio Cesar, Bosingwa, Samba, Hill, Traore, Mbia, Granero (Jenas 46), Mackie, Taarabt, Townsend (Hoilett 72), Zamora (Remy 61).
Subs Not Used: Green,Park, Wright-Phillips, Onuoha.
Man Utd: De Gea,Da Silva, Ferdinand, Vidic, Evra, Nani, Carrick, Giggs, Young (Valencia 67), van Persie (Welbeck 41), Hernandez (Rooney 61).
Subs Not Used: Lindegaard, Evans, Anderson, Cleverley.
Goals: Da Silva 23, Giggs 80.
Referee: Anthony Taylor

No comments:

Post a Comment