Arsene Wenger
akiwashambulia wakosoaji wake katika mkutano wake na wana habari jana
jumatatu.
|
‘Mtanikumbuka nitakapo ondoka.’ meneja huyo anayekalia kuti kavu alionekana kupandwa na ghadhabu pale alipoulizwa juu ya ripoti kuwa amepewa mkataba wa nyongeza.
Akiongea siku moja kabla ya mchezo wa leo wa ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich, Wenger alitetea rikodi yake akisema
‘Nina uhakika utanikumbuka nitakapo ondoka. Angalia timu ninazo weza kuwa meneja nitakwambia siku moja.’
wapinzani wa Arsenal
Bayern Munich wakifanya mazoaezi katika uwanja wa ugenini wa usiku wa
jana.
Arsenal hii leo watakuwa wakikabiliana na Bayern, ambao wanaongoza ligi kuu ya nchini Ujerumani (Bundersliga) kwa utofauti wa alama 15 ikiwa ni siku tatu tu zimepita baada ya Arsenal kuchapwa na Blackburn katika mchezo wa michuano ya FA katika uwanja huohuo wa Emirates.
Wenger anakabiliana na shinikizo la mashabiki wakitaka aondokea kwa kushindwa kupata moja kati ya mataji makubwa tangu mwaka 2005 waliposhinda kwa mara ya mwisho taji la FA huku mwenyewe akijibu tuhuma hizo kwa kusema amekuwepo hapo kwa miaka 16 na malengo yake yamekuwa ni zaidi ya yalivyokuwa hapo kabla.
wachezaji wa Arsenal jana
jumatatu walifanya mazoezi katika kituo cha Colney
Wenger akiongea na
nyota wake Jack Wilshere wakati wa mazoezi.
'Ukisema kazi yangu mbaya ni uongo kama utafanya hesabu zako vizuri.’
Kuhusu Arsena ilivyokabiliana na Blackburn, Wenger ameongeza kwa kusema.
"Watu wanasema sikuwa makini na michuano ya FA laikini wakumbuke nimeshinda hili taji mara nne hebu nitajie ni meneja yupi mwingine aliyeshinda taji hili mara nne.
Si kweli kusema kuwa nilipanga kikosi dhaifu kwasababu nilijaza wachezaji 11 wa kimataifa.
Blackburn wamewatoa
Arsenal kwenye michuano ya FA ikiwa ni miezi 12 cha kupokea kichapo cha mabao
7-1 katika dimba la Emirates.
Watu watasema hiyo siyo fursa nzuri wanataka mataji tu kwa sasa, watasema pengine wanataka mataji ni kweli kwasababu nina timu nzuri.
No comments:
Post a Comment