Pages

Sunday, January 27, 2013

YANGA KAMA SIMBA YAIFUNGA PRISON MABAO 3-1, YAENDELEA KUSHIKILIA USUKANI, DOMAYO AUGUA GHAFLA KABLA YA MCHEZO



Timu ya Yanga imeifunga Prison ya Mbeya mabao 2-1 kwenye mchezo wa ligi unaliochezwa uwanja wa Taifa.
Mabao ya Yanga yamefungwa na Jerry Tegete kipindi cha kwanza na lingine kipindi cha pili na tatu limefungwa na Mbuyi Twite kipindi cha pili.
Lile la Prison lilifungwa na Elias Maguri baada ya kuwazidi mbio mabeki na kufanikiwa  kusawazisha bao.

Mapema kabla ya mchezo  kiungo wa Yanga, Frank Domayo alipatwa aliugua ghafla na jina lake kutolewa kwenye kikosi cha kwanza na nafasi yake ikachukuliwa na Nurdin Bakari na Prison ilipata pigo pale mshambuliaji mpya Emmanuel Gabriel alipoenguliwa kwenye kikosi cha kwanza na nafasi yake kuchukuliwa na Elias Maguri, kwa sababu ya kutokuwa na leseni ya TFF ya kumruhusu kucheza Ligi Kuu.

Kikosi cha Yanga; Ally Mustafa ‘Barthez’, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Simon Msuva, Nurdin Bakari, Didier Kavumbangu, Jerry Tegete na Haruna Niyonzima.

TZ Prisons; David Abdallah, Aziz Sibo, Henry Mwalugala, Lugano Mwangama, Jumanne Elfadhil, Nurdin Issa, Sino Augustino, Freddy Chudu, Elias Maguri, Misango Magai na Jeremiah Juma.

No comments:

Post a Comment