Pages

Friday, January 18, 2013

TANZANIA YAPAA NAFASI SITA BAADA YA KUIFUNGA ZAMBIA DESEMBA MWAKA JANA

TANZANIA imepanda kwa nafasi sita kwenye viwango vya ubora vinavyotolewa  na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kutoka nafasi ya 130 iliyokuwepo mwezi uliopita mpaka nafasi ya 124.
 
Timu tano bora kwa upande wa dunia zote zimebaki katika nafasi zao waliokuwepo mwezi uliopita ambapo wanaongoza na Hispania inayoshika nafasi ya kwanza ikifuatiwa na nchi za Ujerumani, Argentina, Italia na anayefunga orodha ya tano bora ni Colombia.
 
Kwa upande wa Afrika, Ivory Coast imeendelea kuongoza huku ikishika nafasi ya 14 kwa upande wa dunia, ikifuatiwa na Algeria inayoshika nafasi ya pili pamoja na kuporomoka kwa nafasi tatu mpaka ya 24 kwa upande wa dunia.
 
Nchi zingine za Afrika ni Mali iliyobaki katika nafasi yake ya 25 waliyokuwepo mwezi uliopita wakifuatiwa na Ghana waliopanda kwa nafasi nne mpaka nafasi ya 26 na tano bora kwa upande wa Afrika inafungwa na mabingwa wa Afrika Zambia ambao wamekaa katika nafasi ya 39 baada ya kuanguka kwa nafasi tano.

No comments:

Post a Comment