LULU AKIWA NA USO WA MACHOZI YA FURAHA BAADA YA KUACHIWA
Msanii Elizabeth "Lulu" Michael tayari amerudi uraiani baada ya kuachiwa kwa
dhamana katika mahakama kuu jijini Dar. Licha ya kukamilisha kwa
masharti yote aliyopewa jana ikiwa ni pamoja na kutoa milioni 20 kwa wadhamini
wawili, kuripoti kila mwanzo wa mwezi na kuacha hati yake ya kusafiria
mahakamani hapo, Lulu hakufanikiwa kutoka kwa kile
kilichoripotiwa kutokuwepo kwa msajili , hivyo kumlazimu kurudi
gerezani
Lulu
(katikati) akiwa mwenye majonzi na furaha hapa akitokwa na machozi wakati
msemaji wa familia Msanii Dr Cheni akizungumza . Lulu amewaomba watanzania wote
wamuombee maana hii ni dhamana tu na kesi yake bado
inaendela.
LULU na Mama yake mzazi ndani ya gari
tayari kwa safari ya kurudi nyumbani
Wakili
wake Ndugu Flugence Massawe amesema kwamba hii ni hatua ya kwanza kwasababu case
bado inaendelea. Kwa sasa wanasubiri mahakama itoe tarehe ya Lulu kurudi
mahakamani.
No comments:
Post a Comment