Pages

Sunday, January 27, 2013

JOTO LA UCHAGUZI WA SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI LAANZA, WAGOMBEA WA NAFASI ZA JUU WAWEKEWA PINGAMIZI

WAGOMBEA wanaowania nafasi za juu na ujumbe za uongozi wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) na Bodi ya Ligi Kuu wamewekewa pingamizi na wadau mbalimbali wasigombee nafasi walizoomba.

Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah ambaye ni Katibu wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, amewaambia Waandishi wa Habari kwamba, jumla ya pingamizi 14 zimewasilishwa tangu  zoezi hili  lilipoanza na kuhitimisha jana.

Wagombea waliowekewa pingamizi ni Jamal Malinzi, Athumani Nyamlani wanaogombea Urais wa TFF, Michael Wambura anayegombea nafasi ya makamu.

Pia Angetile alisema kwamba upande wa Bodi ya Ligi Kuu, wagombea Yussuf Manji, Ahmad Yahya Juma na Mohamed Said anayegombea nafasi ya makamu wamewekewa pingamizi pia.

Aidha, wagombea wa nafasi za Ujumbe, Epatha Swai, Eliud Mvella na Athumani Kambi wamewekewa pingamizi.

Nyamlani amewekewa pingamizi mbili, moja na Mtanga Yussuf Gacha na nyingine ya Menard Justinian, wakati Malinzi amewekewa pingamizi moja na Agape Fuwe. Wambura yeye amewekewa pingamizi mbili, moja ya Osiah Samuel Msengi na Saidi Rubeya.

Wajumbe Epatha Swai amewekewa pingamizi na Ramadhan Sesso na Sos Chalamila, Eliud Mvella amewekewa pingamizi na Saidi Kiponza, Abdul Changawa na Peter Namengi, wakati Athumani Kambi yeye amewekewa pingamizi na Jeremiah John Wambura

Manji amepingwa na watu wawili ambao ni mwanachama maarufu wa Simba, Daniel Tumaini Kamna na mwingine ni mwanachama wa Yanga, Juma Ally Magoma, Frank Mchaki amepingwa Ahmad Yahya na Mohamed Said.

Kamati itakutana jumatano kujadili pingamizi hizo na inawakumbusha wote waliowekewa pingamizi kufika ofisi za TFF saa 4:00 asubuhi siku hiyo kusikiliza pingamizi zao pia na walioweka pingamizi.

No comments:

Post a Comment