Pages

Sunday, January 27, 2013

HUKUMU YA KIFO KWA WATU 21 YA MAHAKAMA NCHINI MISRI YASABABISHA VURUGU TENA, WACHEZAJI WAWILI WAPOTEZA MAISHA

WADAU wa soka nchini Misri wako katika maombolezo baada ya mchezaji wa Marek Mahmoud Abd Al Halem na golikipa wa zamani wa Al Masry, Tamer Fahalawas kuuwawa katika vurugu zinazoendelea huko Port Said.

Watu zaidi ya 30 wameuwawa Port Said kuanzia jumamosi katika mapigano ya waandamanaji na vikosi vya usalama vya eneo hilo, vurugu ambazo zilizuka baada ya Mahakama nchini humo kuwahukumu kifo watu 21 ambao walihusika katika vurugu zilizoua watu 74 katika mchezo wa soka kati ya Al Masry na Al Ahly.

Mashabiki wa timu zote mbili ambao wanajulikana kama Ultras wanadai kuwa polisi nao walihusika kwa kiasi kuchangia vifo vilivyotokea Port Said na kumlaumu rais wa Misri Mohammed Morsi kwa kushindwa kulisuka upya jeshi hilo.

Mwenyekiti wa Merekh Morsy Sarhan alithibitisha kifo cha Abd Al Halem ambaye alijiunga na timu hiyo miezi michache iliyopita ambapo tukio hilo lilimkuta wakati akielekea mazoezini. Sarhan aliongeza kuwa wataomboleza kifo cha mchezaji huyo kwa siku tatu ambaye alipigwa risasi pamoja na kutokuwa na hatia na kuwataka watu kuheshimu maamuzi ya mahakama ili maisha ya mchezo wa soka nchini humo yarejee kama kawaida.

No comments:

Post a Comment