Meneja Mahusiano wa Multichoice Tanzania Barbara Kambogi (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Mkurugenzi wa MultiChoice Africa kwa ukanda wa Afrika Mashariki Stephen Isaboke ambapo amesema Wateja wa huduma za Dstv nchini Tanzania wametakiwa kutokuwa na hofu ya kupata muingiliano au kukatika kwa picha katika kipindi hichi cha kutoka analogia kwenda digitali
Barbara
Kambogi amesema watanzania ambao wamejiunga na Dstv hawatahitaji kuhama
kwa kuwa Dstv iko katika mfumo wa digital tangu awali
Ameoneza
kuwa Dstv imekuwa ikitoa huduma za digital televisheni kwa Tanzania kwa
kipindi cha miaka 17 iliyopita, ambapo wateja wake wameweza kupata
channel nyingi zaidi za kuchagua zikiwa na picha safi na sauti bora.
Kupitia
vifurushi tofauti vinavyotolewa na Dstv wateja wanakuwa na maamuzi ya
kuchagua kifurushi anachotaka na bei ambapo Ofa ya msimu wa Sikukuu za
Krismas inaendelea pamoja na punguzo la asilimia 10 la kufanya malipo
kabla ya muda uliolipia huduma kumalizika. Kulia ni Operation Manager wa
Multichoice Tanzania Bw. Ronald Baraka Shelukindo.
Operation
Manager wa Multichoice Tanzania Ronald Baraka Shelukindo akifafanua
jambo kuhusu Televisheni nyingine kuingizwa katika huduma za DStv na
kusema suala hilo litategemeana na makubaliano na mikataba na wamiliki
pamoja na kutegemea uwezo wa Satelite.
Kwa
Tanzania DStv inamkataba na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) la
kuichukua TBC katika DStv Platform ambapo itakuwa inaonekana bure hata
kama hujalipia king’amuzi chako chaneli hiyo haikatwi.
Bw.
Shelukindo amewataka Watanzania kuendelea kununua ving’amuzi vya DStv
kabla ya kuisha kwa Ofa ya msimu wa Sikukuu za Krismas na Mwaka mpya.
No comments:
Post a Comment