Pages
▼
Thursday, January 10, 2013
AZAM FC YAFUZU FAINALI ZA MAPINDUZI CUP, YAIFUNGA SIMBA PENALTI 5-4
Mabingwa wa Kombe la Mapinduzi Azam FC jana usiku ilifanikiwa kutinga fainali za mashindano hayo baada ya kuifunga Simba SC kwa penati 5-4 katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa kwenye Uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar.
Azam ambao walikuwa pungufu walifanikiwa kufuzu kucheza fainali baada ya dakika 120 kumalizika kwa sare ya 2-2 na kulazimika kupigwa penalti na mchezaji wa Azam FC Malika Ndeule alipiga penati ya ushindi huku Haruna Athumani wa Simba akikosa.
Hii ni mara ya pili kwa Azam FC kuitoa Simba katika nusu fainali ya Mashindano hayo, mwaka jana Azam FC iliifunga Simba 2-0 katika nusu fainali uliyochezwa uwanja huo.
Penati za Azam FC ziliwekwa wavuni na Gaudence Mwaikimba, Himid Mao, Jockins Atudo, Haji Nuhu na Malika Ndeule upande wa Simba zilifungwa na Miraji Madenge, Jonas Mkude, Miraji Adam na Ramadhan Kipendamoto.
Baada ya matokeo hayo Azam FC inasubiri kucheza na mshindi wa mechi ya Tusker FC ya Kenya na Miembeni utakaochezwa katika uwanja huo.
Katika mchezo huo Azam FC walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 9 kupitia kwa mchezaji Humphrey Mieno aliyefunga kwa kichwa akimalizia mpira wa kona iliyopigwa na Ibrahim Mwaipopo.
Wachezaji wa Azam FC walimaliza kipindi cha kwanza wakiwa mbele kwa goli moja bila dhidi ya Simba, mchezo huo ulisimama kwa dakika nne katika kipindi hicho baada ya umeme kukatika uwanjani, ulikatika dakika ya 14-19 uliendelea tena.
Kipindi cha pili Simba walisawazisha bao hilo katika dakika ya 77 kupitia kwa mchezaji Rashid Ismail aliyepiga shuti la mbali lililokwenda moja kwa moja wavuni, goli la pili lilifungwa dakika ya 109 na mchezaji Miraji Madenge.
Timu zote zilifanya mabadiliko upande wa Simba waliingia Emily Mgeta, Isihaka Hassan, Miraji Madenge, Said Demla kuchukua nafasi za Ramadhan Singano, Abdalah Seseme, Marcel Kacheza na Athmani Hassan Khatibu.
Pia Azam FC walifanya mabadiliko walitoka Seif Abdalah, Brian Umony na Humphrey Mieno nafasi zao zilichukuliwa na Gaudence Mwaikimba, Jabir Aziz na Malika ndeule.
Katika mchezo huo wachezaji wawili wa Azam FC walionyeshwa kadi nyekundu ambao ni Ibrahim Mwaipopo dk 108 alionyeshwa kadi mbili za njano na Jabir Aziz alimtendea madhambi Emily Mgeta wa Simba katika dakika ya 115.
Mchezaji Atudo dakika 119 aliisawazishia Azam FC bao kwa mkwaju wa penati iliyoamriwa na mwamuzi Sheha baada ya beki wa Simba Emily Mgeta kumwangusha Malika katika eneo la hatari, na kupelekea matokeo ya 2-2.
Azam FC Mwadini Ally, Himid Mao, David Mwantika, Atudo, Michael Bolou, Seif Abdala, Ibrahim Mwaipopo, Brian Umony,Malika Ndeule, Humphrey Mieno.
Simba William: Mweta, Miraji Adam, Paul Ngalema, Hassan Hatibu, Komabil Keita, Jonas Mkude, Ramadhan Singano, Abdalah Seseme, Marcel Kacheza na Haruna Athman.
No comments:
Post a Comment