Pages

Thursday, January 10, 2013

ASHANTI UNITED YATOKA SARE NA UKONGA UNITED


Jamali Hilal wa Ukonga akimzuia mshambuliaji wa Ashanti Khan Alex wa Simba wakati wa mchezo wa kirafiki uliochezwa jana kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Ilala

 
Mshambuliaji wa UkongaThamas Lucas akimpiga kanzu beki wa Ashanti United Hassan Othman wakati wa mchezo wa kirafiki uliochezwa leokwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Benjamini Mkapa Ilala 

Mshambuliaji wa Ukonga Jamal Hilal akimtoka mchezaji wa Ashanti United Khan Alex wakati wa mchezo wa kirafiki uliochezwa uwanja wa Benjamini Mkapa, Ilala



Timu ya Ashanti United inayoshiriki ligi daraja la kwanza leo imelazimishwa sare ya 1-1 na timu ya Ukonga United ambayo ipo daraja la pili, mchezo uliochezwa uwanja wa Shule ya Sekondari Benjamini Mkapa Ilala.

Mchezo huo ambao ulikuwa wa ushindani ulishuhudi timu zote zikienda mapumziko bila kufungana.

Kipindi cha pili kialianza kwa timu zote kufanya mabadiliko hali iliyofanya ngome za timu zote kuwa ngumu kuingilika.

Ukonga United walijipatia bao dakika ya 75 kupitia kwa Jamal Hilal baada ya kuwazidi mbio mabeki wa Ashanti na kupiga shuti lililomshinda mlinga mlango wa Ashanti Ibrahim Himidi.

Dakika ya 82 Lusajo Emanuel aliwainua mashabiki wa Ashanti waliokuwa wametulia kama maji ya mtungi baada ya kusawazisha bao kupitia mpira wa adhabu kubwa.

Baada ya mchezo kumalizika kocha wa Ashanti Mubaraka Hassan alisifu kiwango cha wapinzani wao na kusema wameonyesha mchezo mzuri jambo linalosaidia kupima kikosi cha baada ya mapumziko ya kuanza mzungukon wa pili wa ligi daraja la kwanza.

"Timu yangu imecheza vizuri lakini pia Ukonga wamecheza vizuri hali ambayo inasaidia kujua mapungufu yapo wapi na kuyafanyia kazi kabla mzunguko wa pili haujaanza", alisema Mubaraka

Timu ya Ashanti United inacheza ligi daraja la kwanza na inaongoza ligi kwenye kundi B kwa kuwa na pointi 15.

No comments:

Post a Comment