Pages

Friday, January 18, 2013

52 WACHUKUA FOMU KUGOMBEA UONGOZI TFF NA 50 WAREJESHA. ZOEZI LAFUNGWA RASMI SAA KUMI JIONI. KAMATI YA LYATO KUANZA KUZIPIA KESHO

 





Zoezi la kuchukua na kurejesha fomu za kuwania uongozi katika shirikisho la soka nchini tayari limefungwa ambapo jumla wa watu 50 kati ya 52 waliochukua fomu kuomba kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa huo utakaofanyika Februari 24 mwaka huu wamerejesha fomu hizo.
 
Waombaji ambao hawakurejesha fomu ni Geofrey Nyange aliyekuwa akiomba ujumbe wa Kamati ya Utendaji kuwakilisha mikoa ya Morogoro na Pwani, na Shufaa Jumanne aliyekuwa akiomba kuwakilisha Kanda ya Dar es Salaam.

Orodha kamili ya waombaji ambao wamerejesha fomu ni Athuman Nyamlani, Jamal Malinzi, Omari Nkwarulo na Richard Rukambura (Rais). Michael Wambura, Ramadhan Nassib na Wallace Karia (Makamu wa Rais).

Kwa upande wa ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Abdallah Musa, Salum Chama na Kaliro Samson (Kagera na Geita), Jumbe Magati, Mugisha Galibona, Richard Rukambura, Samuel Nyalla, Titus Osoro na Vedastus Lufano (Mara na Mwanza).

Epaphra Swai na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo, Elly Mbise na Omari Walii (Arusha na Manyara), Ahmed Mgoyi na Yusuph Kitumbo (Kigoma na Tabora), Ayubu Nyaulingo, Blassy Kiondo, Nazarius Kilungeja na Selemani Kameya (Katavi na Rukwa) na James Mhagama na Stanley Lugenge (Njombe na Ruvuma).
 
Athuman Kambi, Francis Ndulane na Zafarani Damoder (Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na Stewart Masima (Dodoma na Singida), Farid Nahdi, Hassan Othman Hassanoo, Riziki Majala na Twahili Njoki (Morogoro na Pwani), David Lugenge, Elias Mwanjala, Eliud Mvella na John Kiteve (Iringa na Mbeya), Davis Mosha, Khalid Mohamed na Kusiaga Kiata (Kilimanjaro na Tanga) na Alex Kamuzelya, Juma Pinto, Muhsin Balhabou, Omari Abdulkadir na Shaffih Dauda (Dar es Salaam).

6 WAOMBA UONGOZI BODI YA LIGI KUU, WOTE WAREJESHA FOMU
Waombaji wote sita wa uongozi katika Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) ambayo uchaguzi wake utafanyika Februari 22 mwaka huu wamerejesha fomu.

Kwa upande wa Mwenyekiti waombaji ni Hamad Yahya wa Kagera Sugar na Yusuph Manji wa Yanga wakati Makamu Mwenyekiti aliyeomba ni Said Mohamed wa Azam.

Nafasi mbili za ujumbe wa Bodi ya Ligi Kuu kwa klabu za Daraja la Kwanza zimeombwa na watu watatu. Waombaji hao ni Christopher Peter Lunkonde wa Moro United, Kazimoto Miraji Muzo wa Pamba ya Mwanza na Omari Khatibu Mwindadi.

Kamati ya Uchaguzi ya TFF itaanza kukutana kesho kwa ajili ya kupitia fomu zote zilizowasilishwa na waombaji kwa ajili ya uchaguzi wa TFF na ule wa Bodi ya Ligi Kuu.

Pia Kamati inapenda kuwakumbusha waombaji uongozi kuzingatia Kanuni za Uchaguzi, kwani baadhi yao wameanza kufanya kampeni kupitia vyombo vya habari. Kwa walioanza kufanya kampeni kabla ya wakati wanajiweka katika hatari ya kuenguliwa kushiriki katika uchaguzi.

No comments:

Post a Comment