Bao la Tusker lilipatikana katika dakika ya 44 ya mchezo likifungwa na Ismail Dunga kwa njia ya penati baada ya mwamuzi Oden Mbaga kuamuru penati iliyotokana na kiungo Nurdin Bkari kumwangusha katika eneo la hatari Aucho Khali.
Katika mchezo huo Yanga inayofundishwa wa kocha wake Ernstus Brands iliwatumia wachezaji wake watatu iliyo waongeza katika usajili wa dirisha dogo akiwemo Kabange Twite na wachezaji vijana waliopandishwa kutoka kikosi cha pili Rehani Kibingu na George Banda ambao walionyesha uwezo wa kuridhisha licha ya kucheza kipindi cha kwanza kabla ya kutolewa mapumziko.
Baada ya mchezo huo Yanga sasa inajiwinda na safari ya wiki mbili nchini Uturuki ikiwa sehemu yake ya maandalizi ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara, safari ambayo imepangwa kufanyika kabla ya mwaka mpya.Tusker ilingara na wachezaji wake kama George Opiyo, Luke Ochieng, Joseph Shikokoti, Ismail Dunga na Robert Omonuk.
No comments:
Post a Comment