Pages

Saturday, December 15, 2012

VIJANA JAZZ WAIBUKA UPYA, WAIPUA MBILI KALI *Wamshukuru Rais Kikwete kwa kuwapatia vyombo vipya *Zilipendwa zao zakonga mashabiki Masae Bar, Kawe




Picha tofauti za wanamuziki wa Vijana Jazz wakiwajibika jukwaani katika ujio mpya wa bendi hiyo
BAADA ya kuwa 'juu ya mawe' kwa muda mrefu, bendi ya muziki wa dansi ya  Vijana Jazz,  'Wana Air Pambamoto' imeibuka upya kuanza kupiga muziki kwenye kumbi za starehe, huku ikiwa imepua vibao viwili vipya kusuuza nyoyo za mashaki wake.

Ikipiga kwa mara ya kwanza kwenye ukumbi wa Masae Bar, Kawe wilaya ya Kinodoni jijini Dar es salaam, usiku wa kuamkia leo, bendi hiyo imedhihirisha kwamba mashabiki wake wengi bado wapo.

Kwenye ukumbi huo unaotazamana na kilichokuwa kiwanda cha kusindika nyama cha Tanganyika Packers, Vijana Jazz ilithihirisha kuwa 'bado wamo', kwa kupiga nyimbo zake za zamani zikiwemo 'Mary Maria', 'Mwsiho wa mwezi', 'Ngapulila' na 'mawifi', zilizopigwa enzi za muasisi wa bendi hiyo,  marehemu Ahmed Maneti katika miaka ya 1980.

Nyimbo hizo ziliwafanya mashabiki wa bendi hiyo, kucheza kwa hamasa kubwa huku baadhi yao wakifuatisha kuimba samba mba na wanamuziki waliovuokuwa wakiimba jukwaani na wengine kwenda jukwaani kutuza waimbaji.

Licha ya kuonyesha kuwa bendi hiyo bado ni mahiri,  wanamuziki wa zamani iliobaki nao ni Roshi Mselela, Nuru Mhina (Baby White) na viongozi wa bendi Abdallah Mgonahazelu (Katibu) na Saburi Athuman ambaye ni kiongozi wa bendi.

Vibao vibya ambavyo bendi hiyo imeipua ni  'Utanieleza nini', utunzi wake kiongozi huyo na Kina mama wanaweza  uliotungwa na Mgonahazelu.
Athumani alisema, nyumbo hizo zimesharekodiwa na hivi karibuni zitaanza kuingizwa sokoni, lakini akasema bendi yake itafanya hivyo baada ya kuzipiga mara nyingi majukwaani na kuzoeleka masikioni kwa mashabiki wao.

Alisema wakati kazi ya kuzirekodi nyimbo hizo kwa ajili ya kusikilizwa, imeshakamilika, sasa bendi ipo katika jitihada za kuzirekodi katika video ili ziweze kurushwa kwenye vipindi vya Televisheni na pia kuuzwa kwa mashabiki.

"Tunamshukuru Rais Jakaya Kikwete ametutoa juu ya mawe, hivi vyombo mnavyoona ametuwezesha mheshimiwa Kikwete. Kwa kweli tunamshukuru sana", alisema Mgoma Hazeru wakati kabla ya bendi hiyo kuanza kuiba wimbo wao mpya wa 'Utanieleza nini'.

Mratibu wa Budurani zote kwenye ukumbi wa Masae, Juma Mbizo, amesema atakuwa anazitumia kutoa burudani kwa mashabiki. Nyingine ni kama Msondo Band na FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma'.

No comments:

Post a Comment