Pages

Monday, December 17, 2012

VESPER BONANZA LATIA FORA VIWANJA VYA BORA, JIJINI DAR ES SALAAM

Nahodha wa Shein Rangers Flowin Hondole akikabidhiwa kombe na Mkurugenzi wa kamapuni ya ulinzi ya Vesper Richard Dittmer ambayo ndio wadhamini wa mashindano hayo kwenye uwanja wa Bora Kijitonyama, jijini Dar es salaam

Shein Rainger wakiwa pamoja na uongozi na makobe waliyotwaa

TIMU ya Shein Rangers,leo imeibuka kuwa mabingwa wa bonanza la Vesper lililofanyika kwenye uwanja wa Bora Kijitonyama, jijini Dar es salaam.

Bonanza hili lilishirikishab timu nane za wachezaji waliochini ya miaka 12 ambazo zilikuwa kwenye makundi mawili ya timu nne kila kundi.

Shein imeibuka mabingwa baada ya kuifunga Makumbusho mabao 3-0, yaliyotiwa kimiani na Omari Juma dakika ya 7, Bashilu Said dakika ya 10 na Flowin Hondole dakika ya 20.

Bingwa walikabidhiwa kombe kubwa huku mchezaji bora Seleman Hamidu toka Vesper akipewa kombe ndogo, mfungaji bora Bashiri Said wa Shein Rangers pia akipewa kikombe kidogo na zawadi ya kipa bora kadhalika ilikwenda kwa Shein Rangers.

Timu zilizoingia nusu fainali ni Vesper, Bonde FC, Shein Rangers na M

No comments:

Post a Comment